NINI KIMEJIRI DUNIANI

OSAMA BIN LADEN AUAWA

Osama Bin Laden
Mwanzilishi na kiongozi wa kundi la kigaidi la Al Qaeda Osama Bin Laden ameuwawa na majeshi ya Marekani nchini Pakistan, rais Obama amesema.
Kiongozi huyo wa al-qaeda aliuwawa katika operesheni ya ardhini nje ya mji wa Islamabad kwa mujibu wa taarifa za kijasusi.
Bw Obama amasema baada ya ufyatulianaji wa risasi, majeshi ya Marekani ilichukua mwili wake.
Bin Laden anashutumiwa kwa kuhusika katika baadhi ya vitendo vya ukatili ikiwemo mashambulizi mjini New York na Washington, mnamo Septemba 11, 2001.
Kifo chake ni pigo kubwa kwa kundi la al-qaeda lakini kuelezea hofu kuwa huenda wakashambuliwa katika mashambulizi ya kulipiza kisasi.
Bw Obama anasema alielezea Agosti, mwaka uliopita, kuhusu kule Osama Bin Laden amejifisha. Kufuatia uchunguzi wa ujasusi waligundua amejificha mjini Pakistan.

Wiki iliyopita rais Obama alitoa amri kwa operesheni kufanyika ''kumsaka Bin Laden'' . Bw Obama amesema operesheni hiyo iliendeshwa na kundi ndogo la wanajeshi wa Marekani katika eneo la Abbottabad, Kaskazini mwa Islamabad.

''Baada ya ufyatulianaji wa risasi, Bin Laden aliuwawa na mwili wale kuchukuliwa na majeshi ya Marekani'' rais Barack Obama amesema. 
(habari  kutoka bbc)


                                                                                                                                                                  

HUKO LIBYA  TENA

Gaddafi anataka mazungumzo


Kiongozi wa Libya, Kanali Gaddafi, ametoa wito kwa Nato kwamba kufanywe mazungumzo ili kusimamisha mashambulio ya ndege za umoja huo dhidi ya nchi yake.


Katika hotuba iliyotangazwa kwenye televisheni, Kanali Gaddafi alisema yeye yuko tayari kusimamisha
 mapigano ikiwa itakubaliwa na pande zote.
Mlibya anatazama hotuba ya Kanali Gaddafi
Katika hotuba yake Jumamosi asubuhi, kiongozi wa Libya alisema yuko tayari kutoa amri kuwa mapigano yasitishwe na kuanza mazungumzo, endapo NATO itaacha mashambulio ya mabomu.
Lakini alikataa lile dai kubwa la wapiganaji na jumuiya ya kimataifa, kwamba yeye aondoke.
Alisema hatong'atuka wala kuihama Libya.
Wengi serikalini wanaona kuwa wameshakaribisha mazungumzo kwa kukubali mpago wa Umoja wa Afrika wa kurejesha amani; lakini wanahisi upinzani ndio hautaki kumaliza mapigano, kwa sababu unakataa kuzungumza na serikali ya Kanali Gaddafi.
Alipokuwa Kanali Gaddafi anazungumza, NATO ilidondosha makombora matatu mjini Tripoli, kwenye yale yaliyoonekana kama majengo ya serikali.
Hotuba ya Kanali Gaddafi, ilikuwa mchanganyiko wa kukaza na kulegeza kamba.
Alisema kila mwananchi wa Libya sasa anakabili mambo mawili : uhuru ama kifo.
Hakuna kusalliam amri, hakuna hofu wala kuondoka.

Post a Comment

17 Comments

Anonymous said…
ahsante kwa kutuhabarisha mambo nyeti kaka.
Anonymous said…
maajabu ynaendelea. ila naona kumekucha na hya yaliyo jiri hapa ulimwenguni.
Anonymous said…
nani anauhakika osama amekufa? wamerican wanajipendekeza tu. osama alikufa miaka ya nyuma sana. wemyewe wanajidai wamehusika. wamefulia vibaya hao. kiukweli ni kwamba wasitake kutafuta umaarufu dunian osama kifo chake kilifika na ndio sababu ya yeye kutoweka dunian lakini si mmarekani aliyemua kwani wanajidanga tu. jmani hata aibu hamuoni?
Anonymous said…
Kumbe gadafi anahistoria hivi tena za kutisha mmmmm.
Anonymous said…
ila kiukweli gadafia anamambo ya kiudicteta. na istoshe amekaa madarakani kwa muda mrefu. kunajamaa alishwahi kusema amechoka kula wali kila siku hata kama haumdhuru. kwani anataka kugonga ugali. ilamaana hata libya wanataka rais awe mwingine. si huyo wa siku zote. sasa swali anang'ang'ania nini madaraka? na si haachia kiujula hafai sasa huyo ni rais used anatakiwa new.
Anonymous said…
Me najiuliza hivi kama angekubali kuachia madaraka wananchi wangeandamana nini? kiujumla huyu rais ni member freemasons kwa hiyo alikuwa akitafuta damu. nikiwa na maana kwanini hataki kuachia madaraka. kwani hao watakao shika watashindwa kuongoza utajiri wa libya? kiuju,la huyu jamaa anakaung'ang'nizi ka udini na ubinafsi moyoni mwake.
Anonymous said…
gadafi wamuonea tu na wamarekani ni chanzo. wanatafuta utajiri kwa gadafi.
Anonymous said…
gadafi aspo angalia atakuwa kama sadam hosen. mwisho walimuhukumu kifo. aonewi ila ni ubinafsi na uroho wa madaraka. hakuna mtu anaeweza kukubali kuchukuliwa utajiri wake na kwani alikosa washauri mapaka agome kung'ka madarakani. jibu hakukosa ila tu. ni ka uroho. kwa wivu na chuki. kwanini wengine wapate. na atakufa kama sadam.
Anonymous said…
gadafi haonewi ni uroho wa madaraka tu.
Anonymous said…
gadafi chagua la waislamu. na ndio maana anaonewa.
Anonymous said…
gadafi hana sera kimeo tu.
Anonymous said…
gadafi kweli msimamo anao. lakini wakati ukifika wa kustakiwa watamsaidia?
Anonymous said…
gadafi haana lolote . kumbukeni gadafi kaleta utajiri libya kwa kulinda .
Anonymous said…
wewe. mungu ndio kaleta amani na utajiri. msifagilie binadamu. ila kapewa mamlaka ya kuongoza binadamu wenzie na mwenyezi mungu. na nyie binadamu mkapewa uelewa.
Anonymous said…
osama mwenyewe amekufa ije kuwa gadafi. huyo mtu mdogo tu huyo?
Anonymous said…
libya itakuwa hivyo hivyo kma gadafi htaachia madaraka.
Anonymous said…
gadafi kiboko.