- Dakika 10 zilizopita
Rais
wa Kenya Uhuru Kenyatta amesema yuko radhi kwenda katika mahakama ya
kimataifa ya ICC kwa kikao maalum kuhusu kesi inayomkabili.
Akiwahutubia
wabunge mjini Nairobi,aliwaambia kuwa yuko tayarti kuhudhuria kikao
maalum alichotakiwa kuhudhuria mjini Hague bila wasiwasi wowote.Kenyatta alitakiwa na majaji wa mahakama hiyo kufika ICC tarehe 8 mwezi huu kufafanua madai kuwa serikali yake imekataa kushirikiana na mahakama hiyo hasa upande wa mashitaka kwa kukataa kuipatia ushahidi unaohitajika katika kesi inayomkabili.
Anakabiliwa na tuhuma za kupanga ghasia za kikabila zilizokumba nchi hiyo baada ya uchaguzi wa mwaka 2007/2008.
Aliarifu bunge kuwa anajiamini mwenyewe kiasi cha kuwa tayari kufika mbele ya ICC na kwamba anajua hana hatia katika kesi inayomkabili.
Alisema Kenya ni nchi huru na kwamba haitawahi kuwa chini ya mamlaka nyingine yoyote.
Takriban wabunge miamoja wanajiandaa kuambatana na Kenyatta Hague katika ishara yao ya kumuunga mkono.
Uhuru amemkabidhi mamlaka kwa muda naibu wake William Ruto hadi atakaporejea.
0 Comments