Wakimbizi wafia kambini mpakani Nigeria

Maelfu ya watu wametoroka makwao kutokana na mapambano dhidi ya Boko Haram 
 
Taarifa kutoka nchini Cameroon zinasema kuwa wakimbizi waliotoroka kutoka kwa wapiganaji wa Boko Haram wamefariki wakiwa katika kambi ya wakimbizi.
Baadhi ya wakazi waliokuwa kambini katika mji wa Fotokol karibu na mpaka wa Nigeria, wanasema kuwa mazingira katika kambi hizo, yalikuwa mabaya sana na kwamba watoto walifariki baada ya kuugua Malaria.
Wengine walilalamika kuwepo uhaba wa chakula kambini na kwamba walilazimika kuiba chakula kutoka kwa mashamba ya wenyeji.
Wadadisi wanasema ushirikiano kati ya Nigeria na Cameroon katika kupambana na wapiganaji wa Boko Haram umekuwa mdogo sana licha ya ahadi kutoka kwa viongozi wa mataifa hayo mawili.

Post a Comment

0 Comments