Jua haki yako unapokamatwa na polisi.

  • Raia ana haki ya kumwomba askari ajitambulishe kwako.
    • Mwulize jina lake
    • Mwulize namba yake ya uaskari
  • Raia ana haki ya kujulishwa kwanini anatiliwa mashaka ama kukamatwa.
  • Raia ana haki ya kuwajulisha ndugu, jamaa ama sehemu anakofanyia kazi kwamba ama amekamatwa na polisi ama Taasisi ya Kuzuia Rushwa.
  • Raia ana haki ya kuomba na kupewa dhamana wakati akiwa kituo cha polisi ama Taasisi ya kuzuia rushwa.
    • Hutakiwi kutoa fedha kama dhamana uwapo kituo cha polisi ama Taasisi ya Kuzuia Rushwa, isipokuwa maelezo utakayoandika.
  • Raia ana haki ya kuwaeleza polisi ama Maafisa wa Kuzuia Rushwa kwamba lolote atakalosema linaweza kutumiwa kama ushahidi mahakamani, na asiburuzwe kuandika tu.
  • Raia ana haki ya kuomba Wakili wake awepo kituo cha polisi ama Taasisi ya Kuzuia Rushwa wakati anatoa maelezo yake.
  • Raia ana haki ya kuyasoma kabla ya kutia sahihi yake.
  • Raia ana haki ya kudai risiti ya orodha ya vitu vyake/fedha zake alizozitoa ama kukabidhi kituo cha polisi ama Taasisi ya Kuzuia Rushwa.
  • Raia kama ni mwanamke ana haki ya kupekuliwa na polisi wa kike, na iwapo hakuna polisi mwanamke, basi mwanamke yeyote na vile vile kwa mwanamume.
  • Raia ana haki ya kufikishwa mahakamani katika muda usiozidi saa 24 tangu alipokamatwa na kufikishwa kituo cha polisi.

Post a Comment

0 Comments