Mamia ya Wayahudi wanaofuata
dini yao kiasilia, wamepambana na polisi karibu na Jerusalem kwa sababu
ya mvutano kuhusu kuwatenga wanawake na wanaume.
Makundi ya Wayahudi wanaofuata dini yao kiasili waliwafukuza polisi na kuwarushia mawe.
Ghasia hizo ndio za karibuni kabisa katika mfululizo wa matukio mengine nchini Israil, ambapo wanawake walilazimishwa kukaa nyuma kwenye mabasi, katika maeneo ya Wayahudi hao, ingawa mahakama yametoa amri kuwa wanaweza kukaa watakapo.
0 Comments