Maeneo ya sinza. |
Kiukwe naweza kusema hii imekuwa kero kubwa sana maeneo ya sinza kuanzia hapa kijueni kurudi nyuma kamaunarudi pande za magomeni kiukweli barabara ni mbovu !! mbovu!! mbovu!!! kupita kiasi. hii ni kasumba kubwa sana. na ukiuliza. kwanini barabara wakazi wa maeneo hayo. wanakwambia wamechoshwa na ahadi za viongozi wao. kitaswira na kimuonekano ni kwamba viongozi wetu pale wanapotaka kura zenu. utumia neno la kusema hivi. barabara juu na chini. ili tu wananchi waamini. lakini sasa imekuwa kero sana hasa kwa wakazi wa sinza. na ukiuliza je viongozi hao huwa wanapita maeneo hayo. wakazi hao watakujibu ndio. lakini hii inatokana na dharau za viongozi wetu kwa kuwadharau wananchi. viongozi hao wamekuwa wakipita na magari yao ya kifahari yaliyo tokana pesa za wananchi. nakumbuka kipindi cha kampeni kuna kiongozi alitamka neno hili. nitajenga barabra zote kwa kiwango cha lami. na pia barabara za juu. Lakini sasa imekuwa kwamba kama kiongozi atatoa ahadi za uongo. na asitekeleze je wananchi watamuamini tena? jibu ni hapana. kiukweli kama mtu au kiongozi hawezi kutekeleza jambo ni bora asema hivi, nitatoa huduma kwa kadiri nitakavyo weza. aliye yasema maneno hayo ni rais wetu. siwezi kuacha kumtaja maana nisipo mtaja nitakuwa mnafiki... Jamani viongozi inaonyesha hata familiya zenu mnazidanganya hivyo. kama uongo na ahadi kama hivi mtaendelea nazo. kiukweli mnapeleka taifa kubaya sana na si kingine ni kizai kijacho. HII NI CHANGA MOTO KWA VIONGOZI. NAWAOMBA HIZO PAMBA MLIZO WEKA MASIKIONI ZITOENI.
0 Comments