WATAHINIWA 9,726 sawa na asilimia 32 waliofanya mtihani wa kuhitimu
masomo ya darasa la saba mwaka huu na kufaulu , wamekosa nafasi ya
kuendelea na masomo ya Kidato cha kwanza mwakani kutokana na uhaba wa
vyumba 245 vya madarasa kwenye shule za sekondari mkoani Morogoro.
Ofisa Elimu wa Mkoa wa Morogoro, Fatma Kilimia, alitoa taarifa juzi
wakati wa kikao cha uchaguzi wa wanafunzi watakaojiunga na kidato cha
kwanza mwakani.
Kilimia alisema kuwa kati ya waliokosa nafasi za kuendelea na masomo ya kidato cha kwanza licha ya kufaulu mitihani yao.
“ Tujipange kuwezesha kujenga madarasa haya ,tusisahau pia suala la
vyoo na nyumba za walimu na ujenzi huu uwe umekamilika kabla ya Februari
mwakani, ili watoto wasichelewe katika masomo yao,” alisema Kilimia.
Alisema wanafunzi walioandikishwa Machi mwaka huu kwa ajili ya
kufanya mtihani walikuwa ni 51,775 kati ya hao wavulana 24,979 na
wasichana walikuwa ni 26,796.
Wanafunzi 869 kati yao wavulana 468 na wasichana 401 walishindwa
kufanya mitihani kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo vifo, utoro na
mimba.
Kwa mujibu wa Ofisa Elimu wa Mkoa huo, wanafunzi waliochaguliwa ni 30,808. Wavulana ni 15,161 na wasichana 15,647.
Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, Halima Dendego, aliwataka wakurugenzi
watendaji kwa kushirikiana na madiwani pamoja na wananchi kutumia muda
mfupi uliobakia kujenga vyumba vya madarasa vinavyohitajika ili
kuwezesha watoto wote waliofaulu kuingia darasani kabla ya muhula wa
mwaka wa masomo kuanza.
0 Comments