Kutokana na uchunguzi uliofanyika na mwangajamii imegundulika kuwa makampuni mengi ya ujenzi tanzania yanatabia ya kunyonya wafanyakazi ili neno kunyonya ni neno la kawaida tu. kwa mfano samaki anayeitwa sangara ambaye ni samaki anaekula samaki wenzake nikiwa na maana ni wale samaki wadogo. hivi majuzi mwangajamii iliweza kutia mguu katika maeneo ya pale upanga jijini dar es salaam kwa kampuni moja inayoitwa mohamed belder limited ambapo bila kujali lolote nilijichanganya na mimi kuomba kibarua cha kubeba zege nia na madhumini nikujua wafanyakazi wanalipwa vipi na ni shilingi ngapi. hatimae niligundua kuwa kiwango cha fedha ni kidogo sana wanaolipwa vibarua wa kawaida kwani hulipwa shilingi 5000 hadi 6000. na nikiwango kidogo sana kwa maisha ya sasa hivi. nahaidi kuweka picha na baadhi ya wafanyakazi katika blog hii hivi karibuni. wadau kaeni mkao wa kula.
0 Comments