Swala la umeme tanzania limekuwa kero. kwani mamilioni ya watanzania wanategemea nishati ya umeme kuendesha mambo yao ikiwemo kuhifadhi bidhaa mbalimbali. lakini leo hii serikali inasubutu kutikisa kiberiti kwa kuwaambia wananchi . @ nchi ipo karibuni kuingia gizani. nikisema hivyo kama mwandishi wa habari hii. inafikia hatua napeleka mawazo yangu nakusema ni bora hata hao waigereza warudi tu kuitawala tanzania tena kwa mara ya pili. nahisi watanzania wengi sasa hivi wamefilisika kutokana na hali ngumu ya maisha. hii nikutokana na mifumo mibovu ya viongozi wa serikali. @ kuna msemo wanakuambia wewe mwananchi ndio serikali hii ni sawa na danganya toto ya kumpa pipi Asilie, maneno hayo yananichoma sana sana. wanatufunga macho na biskuti na wakati tunaweza kuivunja. sasa wakati umefika kwa watanzania kutaka kieleweke. nafahamu kuwa mnatupiga vita sana waandishi wa habari kwa kuwa tunawahabarisha wananchi maovu yenu. Sasa leo hii tunaona shirika la tanesco limegeuzwa kama godoro kodi walipe wao bado mnataka waendelee kutoa huduma. bado Tanesco inawadai nyie vigogo pamoja serikali lakini mnajifanya hamuoni wala hamsikii. Kwa taarifa yenu sasa hivi kila mwananchi anajua kuwa hiyo tanesco haihusiki na umeme ila wahusika ni nyie. Viongozi wasirikali huu mwaka si wa mabwege tena kwa watanzania wengi wamesoma na si enzi la mwalimu nyerere
0 Comments