Benki tatu zimekubali kutoa mkopo wa shilingi bilioni 408 (Dola za
Marekani 256) kwa Shirika la Umeme Tanzania kwaajili ya mpango wa
dharula wa kuzuia kukatika kwa umeme, gazeti la Daily News la Tanzania
liliripoti Jumatatu (tarehe 19 Machi).Fedha hizo zitasaidia kununua
mafuta mazito kwaajili ya mitambo inayotumia mafuta mazito hayo, alisema
William Mhando, mkurugenzi mkuu wa Shirika la Uzalishaji na Ugavi wa
Umeme Tanzania (TANESCO). "Tunatarajia kupata fedha hizo wili lijalo." Kampuni inafanya kazi katika "changamoto ya muda" kukarabati
miundombinu ya umeme nchi nzima, Mhando alisema, aliongeza kwamba
uzalishaji umeshuka hadi megawati 718 kutoka megawati 1200. Alisema
shirika la umeme halifanyi mgao wa umeme na tatizo lolote linatokana na
mfumo mbaya wa miundombinu. "Hakukuwa na uwekezaji madhubuti katika eneo
hili kwa muda mrefu," alisema. City Bank Tanzania, National Microfinance Bank na National Bank of Commerce zinatoa mkopo kwaajili ya mradi huo.
1 Comments