Maafisa wa serikali ya Pakistan, wamesema mshambuliaji huyo wa kujitoa mhanga alifika hapo kwa miguu na kujilipua karibu na kizuizi cha polisi katika eneo linalokaliwa na watu wa kabila la Bajur.
Aidha wamesema walikuwa wakimlenga afisa mmoja mwandamizi wa polisi ambaye ametekeleza mauaji ya raia kadhaa na kuwatia nguvuni idadi kubwa ya wapiganaji wao.
Maafisa wa ulinzi walengwa
Ripoti zinasema mshambuliaji mwenye umri wa miaka chini ya ishirini aliwalenga maafisa hao wa polisi mapema hii leo.Watano kati ya waliouawa ni maafisa wa polisi na miongoni mwao ni afisa mkuu wa polisi katika kizuizi hicho na naibu kamanda wa polisi kutoka kabila hilo ambaye aliajiriwa na serikali, ili kusaidia katika mikakati ya kupambana na wapiganaji wa Taleban Kaskazini Magharibi mwa nchi hiyo.
Katika siku za hivi karibuni, maafisa wa ulinzi nchini humo wamekuwa wakilengwa na wapiganaji wa Taleban na Al-Qaeda.
Eneo hilo la Bajur limeshuhudia makabiliano makali zaidi kati ya wanajeshi wa serikali wanozizatiti kupambana na wapiganaji wa waasi.
Shambulio hilo ndilo mbaya zaidi kuwahi kutokea nchini humo tangu tarehe mbili mwezi Machi mwaka huu, wakati watu 22 waliuawa na mlipuaji wa kujitoa mhanga katika msikiti mmoja katika wilaya ya Khyber.
0 Comments