Mjumbe maalum wa Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa
Afrika (SRCC) nchini Somalia, Balozi Mahamat Saleh Annadif ameshutumu
vikali shambulio la kigaidi lililofanywa leo na magaidi wa Al-Shabaab
katika makao ya Umoja wa Mataifa mjini Mogadishu.
"Tunalaani vikali shambulio hili la kinyama
katika makao ya Umoja wa Mataifa mjini Mogadishu. Mashambulio haya
yasiyofanikiwa yanayoendeshwa na Al-Shabaab yanalenga tu kuvuruga
jitihada zinazochukuliwa na wananchi wa Somalia baada ya vita vya
wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa zaidi ya ishirini na magaidi hao
hawawezi kuzuia jitihada zetu za pamoja kuendelea kuwasaidia wananchi wa
Somalia kuijenga nchi yao" amesema Mwakilishi Maalum wa Mwenyekiti wa
Umoja wa Afrika nchini Somalia (SRCC), Balozi Mahamat Saleh Annadif. kwa habari zaidi BONYEZA HAPA
0 Comments