HONGERA SANA SUDAN
Jamhuri ya Sudan Kusini kwa sasa inashereheklea uhuru wake baada ya kutangazwa rasmi kuwa taifa huru la 54 la bara la Afrika uhuru ambao umepatakina baada ya vita vya miongo kadha. Kulikuwa na mbwembwe na vigelegele kwenye mitaa ya mji wa Juba huku wenyeji wa taifa la Sudan Kusini wa wakipeperusha bendera ya taifa lao jipya. Viongozi kutoka sehemu mbali mbali za ulimwengu walihudhuria sherehe hizo akiwemo rais Omar al-Bashir akisimama na rais wa Sudan Kusini Salva Kiir, ukiwemo pia ujumbe kutoka Umoja wa Mataifa ukiongozwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon. Ban amesema kwamba leo tunashuhudia historia ya kuzaliwa kwa nchi hii jipya.
SAUTI YA KATIBU MKUAA
Na pia Ban aliwaambia watu wa Sudan Kusini:
“Hii ni lazima iwe siku ya hisia na raha kwa watu wote wa Sudan Kusini, lakini pia hii ina maana kwa nchi zote za eneo hili. Mmetoka mbali lakini uhuru utakuwa ni mwanzo tu. Ni lazima muifanye nchi yenu kuwa nchi ya maendeleo na yenye imekomaa kidemokrasia. Hii ndiyo ahadi ya Umoja wa Mataifa ya kuwasaidia. Niko hapa kuonyesha uungwaji mkono wangu na wa Umoja wa Mataifa kwa watu wote hapa.”
Umati uliohudhuria sherehe hizo chini ya jua kali ulishangilia wakati bendera ya Sudan ilipoteremshwa na bendera mpya ya taifa la Sudan Kusini kupandishwa na tarumbeta kupiga wimbo mpya wa taifa
0 Comments