Vurugu ya kugombea maiti imezuka jioni hii eneo la Manzese Tip Top na kusababisha uharibifu wa mali na majeraha kwa waandishi wa habari waliokuwa wakifutailia sakata hilo. Mwandishi wa mtandao huu anapasha kuwa ugomvi huo umezuka baada ya kijana mmoja kufariki katika mazingira ya kutatanisha, kundi moja la familia liliamua kuzika lakini likaibuka kundi la pili kuzuia kuzika maiti hiyo iliyokwisha pelekwa msikitini kwa kuombewa kabla ya kuzika. Kundili hilo lilipiga mawe msikitini na hata polisi walipoingilia kati nao walipigwa mawe, furugu zikaendelea hadi kituo cha polisi Mabibo Mpakani na Manzese Midizini ambako vimeharibiwa kwa mawe. Pikipiki ilichomwa moto, msikiti wa Tawfiq Manzese (pichani chini) nao ulipigwa mawe. Pichani juu ni mwandishi wa gazeti la Sani Christopher Lissa akiwa na jeraha alilolipata katika vurugu hizo na picha nyingine inaonesha jinsi 'kaunta' ya kituo cha polisi ilivyoharibiwa. |
0 Comments