
Nikweli kwamba, maana halisi ya Yatima ni mtoto aliyefiwa na wazazi.
Nenda ikawa kampotezapoteza mzazi mmoja, bado ataitwa Yatima wa mzazi mmoja.
Bila shaka wote twajua yakuwa Watoto hawa pia wanahaki yakuishi, ambayo haki hiyo inasisitizwa na Mungu baba mwenyewe; Kasema Yeye ni baba wa Yatima.
Watoto hawa, baada yakupoteza wazazi nakukosa msaada; hutafuta namna yakuishi.
Wanaposhindwa, kwakukosa mahali pakuishi nakulala, huondoka nakwenda mitaani kujiifadhi.
JAMBO LAKUSHANGAZA !
Kuliko sisi kuungana pamoja kwa pamoja, tuwasaidie Watoto hawa, tunawapa majina mengine kama
" Watoto wa mitaani "
Swali linakujaJe ? " KUNA MTAA WOWOTE UNAOFAHAMIKA, ULIOBEBA UJAUZITO NAKUZAA MTOTO? "
Jibu ni HAPANA.
hawa Watoto wanahitaji pia upendo wa kweli, nakutambuliwa na Jamii. na wanapokosa hayo, Huwasababishia maumivu moyoni; JAMBO ambalo ,kwakutaka kusahau kwa lazma, huwapeleka kuvuta Gundi, Bangi na Pombe.
Je? HATUWEZI KUWASAIDIA HAWA?
Ndiyo... Tunaweza KUWASAIDIA, kwakutumia kidogo kidogo tulicho nacho nakuwapa wao pia.
Kuwaonyesha upendo wa kweli nakuwafundisha maagizo ya Mungu; pia Kuwaonyesha maadhara ya madawa yakulevya.
0 Comments