NINI KIFANYIKE ILI KUONDOKANA NA UKATILI WA KIJINSIA MAJUMBANI?


UKATILI WA MAJUMBANI
Utangulizi

Ukatili wa majumbani ni aina ya tabia inayotumika kujenga uwezo wa mtu mmoja kummiliki mwingine kwa kutumia vitisho na woga, ukatili wa majumbani aghalabu hutokea kwa watu walio na uhusiano wa kimapenzi na hata wale wanaoishi nyumba moja

Magomvi ya nyumbani pamoja na mambo mengine huhusisha kipigo cha wazi au cha kisiri, kuitana majina yasiyofaa, kutumia fedha kwa madhumuni ya kumiliki wengine, kutumia lugha ya matusi, kubaka watoto ndani ya nyumba, kuwamiliki watoto, kutenga na kutumia vitisho.

Aina za ugomvi
Kipigo
Kusukuma, kupiga, kuburuza, kukanyaga, kukaba, ngumi, kuunguzwa, kuvunjwa mikono, kupigishwa kichwa ukutani au sakafuni, na kutumia nyenzo yoyote kama  silaha

Emotional/athari za kihisia au kiakili

Kupiga kelele, kuapiza, kuvunja utu, kuaibisha, kukosoa, kulaumu, kutishia kudhuru, kufungiwa nje ya nyumba, kutishia kuondoka, kushikashika simu ya mwenzio!!!!!!!!.

Kujamiiana

Kubaka/ubakaji ndani ya ndoa, kushikwashikwa kimwili bila ridhaa, kufanya mapenzi kinyume cha maumbile asilia/ridhaa, kutumia nguvu, kujamiiana kwa kukomoa, kutokuwa mwaminifu na ndoa yako, kuingiza vitu sehemu za siri, kukataa kujamiiana kwa salama.

Kiuchumi

Kuzuia hela za familia, kumkataza mwenza kufanya kazi,kumfanya mwenzio awe anaomba fedha za matumizi na au kumpatia kwa masimango, kuomba mshahara wa mwenzio, kutomruhusu mke kuwa na fedha, kutumia mali/fedha za familia bila ridha ya mwingine, kutomruhusu mke kumiliki mali.

Tamko la Kimataifa la Kuondoa Vitendo viovu dhidi ya Wanawake la 1993 linafasiri ukatili wa kijinsia kama kitendo chochote kile ambacho matokeo yake yanamfanya mwanamke aumie kimwili, kisaikolojia na kimapenzi iwe kwa mtu binafsi au kwa umma[1].
Unyanyasaji kijinsia nchini Tanzania bado ni mkubwa kwani mwaka 2007, jumla ya matukio 6,531 ya vitendo vya unyanyasaji kijinsia yalitokea[2]
Ukatili baina ya wanandoa na wasio wanandoa umekithiri sana katika miaka ya karibuni, mwezi Novemba 2007 zilitolewa taarifa kwamba asilimia 50 ya wanawake Tanzania hupigwa kila siku kutoka kwa wenzi wao[3].mbali na hapo katika utafiti uliofanyika mwaka 2006, asilimia 25 ya wanawake waliohojiwa walikiri kufanyiwa ukatili kwa wapenzi wao wasio wanandoa[4] utafiti ambao ni sambamba na ule ulioonyesha kwamba 1 kati ya wanawake 10 amefanyiwa ukatili katika umri wa miaka 15 na mtu asiye mpenzi wake.
ukatili wa kimwili katika ndoa na kwa wapenzi husababisha majeraha madogo ambayo hatimaye hukua na kuwa  makubwa, shirika la afya duniania lilifanya utafiti na kubaini kuwa asilimia 30 ya wahanga wa ukatili huu hupata majeraha makubwa baada ya kupigwa vibaya[5]
Sababu kubwa ya ukatili huu dhidi ya wanawake ni kuwepo kwa mila na desturi ambazo zinalea ushambuliaji na unyanyasaji wa wanawake[6]. Ambapo vitendo hivi hushamiri na kukomaa na hatimaye kuwa kama sehemu ya maisha ya kawaida, upo ushahidi kuwa katika baadhi ya makabila hapa nchini mwanamke kutokupigwa ni ishara mbaya kwamba mumewe hana wivu naye. katika utafiti uliofanyika mwaka 2006, asilimia 60 ya wanawake waliohojiwa walisema  kwamba wanaamini mwanamke kupigwa ni jambo la kawaida[7] tatizo hili ni kubwa kwani ni moja ya changamoto katika kupinga aina hii ya ukatili, changamoto nyingine ni pamoja na kushindwa kutoa taarifa na pia kutokana na shinikizo la jamii au familia kutaka kumaliza mambo kiungwana, wanawake wengine wamearifiwa kufumbia macho ukatili huu ili kunusuaru watoto na au ndoa zao[8] aidha kuogopa waume zao kupelekwa jela iwapo taarifa zitafika kwa vyombo vya dola na waume hao kuchukuliwa hatua za kisheria[9]

Serikali ya Tanzania imekuwa katika juhudi mbalimbali za kutokomeza ukatili wa majumbani, Mwaka 2001 Serikali ya Tanzania ilizindua Mpango wa Taifa wa Kupinga Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto (2001-2015). Hata hivyo mpango huu umekuwa ukisuasua utekelezaji wake kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ya ukosefu wa fedha na mfumo wa msaada wa kisheria ambapo mwanamke mhanga wa ukatili anaweza kuupata. Mwezi Mei 2008, serikali ilichukua hatua nyingine ya kutafuta suluhu ya tatizo la ukatili wa majumbani kwa wanawake kwa kupitisha mfuko Maendeleo wa Umoja wa Mataifa wa Kampeni ya kupinga ukatili dhidi ya wanawake[10], serikali pia imetoa msukumo kwa wanawake kujitokeza kusema hapana dhidi ya ukatili wa majumbani ili kulinda haki zao[11]
hata hivyo kuna makosa mengi ndani ya sheria ya Kanuni za Makosa ya Jinai ambayo hayamlindi mwanamke kikamilifu dhidi ya unyanyasaji kijinsia mfano katika kosa la kubaka ambapo linatumika kwa watu wasiokuwa katika ndoa tu au waliotengana[12], sheria hii imekaa kimya kuhusu ubakaji ndani ya ndoa.
Kuhusu kampeni ya Tunaweza;
Kampeni ya Tunaweza ni kampeni kubwa inayoendelea kidunia ambayo lengo lake kuu ni tukokomeza ukatili dhidi ya Wanawake, na katika ukanda huu wa Afrika Mashariki, kampeni hii imeenea zaidi kwa Tanzania na Kenya kutokana na ukweli kwamba kuna utamaduni wa ukimya na kufumbia macho ukatili huu miongoni mwa jamii. Kampeni  hii ina lengo la kupata wigo mpana wa ushiriki wa jamii iliyo tayari (critical mass) katika kuzuia ukatili dhidi ya wanawake hasa ukatili wa majumbani na ambao pia watakuwa ni chachu ya mabadiliko katika jamii, katika mashirika na taasisi kufikia mwaka 2012
Malengo mahsusi ya kampeni hii ni;
  • Kufanya mageuzi katika imani na desturi katika jamii zinazochagiza ukatili dhidi ya wanawake
  • Kutanua wigo ushiriki mpana wa jamii kusimama kidete na kwa pamoja katika kupinga ukatili dhidi ya Wanawake
  • Kuanzisha vuguvugu la jamii kupinga ukatili dhidi ya wanawake
  • Kuunda mitandao ya kitaifa na kikanda katika kupinga ukatili dhidi ya wanawake

Mikakati ya Kampeni ya Tunaweza;
  • Kuhamasisha waleta mabadiliko 1.6 milioni katika Tanzania

Mleta Mabadiliko ni mtu yeyote anayehiari na anayethubutu

Ø     Kuadilika kitabia kuachana au kupamban  ukatili dhidi ya wanawake
Ø     Kushawishi watu wengine 10 wanaomzunguka

Mpaka sasa kampeni hii imeshafikia watu….


Post a Comment

0 Comments