May 12, 2011




Jamani   ndugu  watanzania  naumiza  kichwa  sana  kwa  kujiuliza.  hii  ni  biashara  huria  au 

vipi.?   naona  mfumo  wa  technology  mpya  ya  kutembea  na  vibanda  vya  biashara.  kama  mnavyoona  hapo  juu.  gari  naweza  kuliita  kibanda  huria  limesababisha  ajali  eneo  la  moroko  hotel  kati  ya  dereva  pakipiki  na  taxi.  ni  baada  tu  ya  mwenye  pikipiki    kukwepa  kugongana  na  gari  hilo aina  ya  kibanda huria.  na  ndipo  akakumbana  taxi  iliyokuwa  ikitokea kariakoo.  na  kibanda  hiki  kilikuwa  kikimkimbia  trafiki police.  kwa  kumwogopa  kuwacheleweshea   biashara  yao  hiyo  huria.  kiukweli  nikwamba  mipango  yake  iligonga  mwamba   ya kumkimbia  trafiki  huyo.  mimi  naona    wabongo  temechokana  kwa  kutembezeana  biashara  majumbani  kwa  kutumia  vibanda  vyenye  matiri  kama  ya   gari.  Nawapa  pole  watanzania  kwa  ugumu  wa   maisha  ya  kila  siku. 






HII KALI SASA. KWA WALOKOLE WENZANGU.

  SHAMPENI  YAZUA  UTATA  KWA WALOKOLE.  HAWA.

KATIKA kukwepa vinywaji walivyodai kuwa na kilevi,  waumini wa kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) lililopo maeneo ya Mazimbu mkoani Morogoro, walitumia soda aina ya Coca Cola badala ya Shampeni katika sherehe ya kuwapongeza maharusi waliofunga ndoa Jumapili iliyopita.

Katika hafla hiyo iliyofanyika ukumbi wa Mambo Club mjini hapa, kabla ya Mchungaji Salvatory Daffi, kuifungua soda hiyo iliyokuwa imezungushiwa maua kibao, aliiombea na kumkabidhi mfunguaji ambaye naye aliipitisha kwa maharusi na wazazi wa pande
zote mbili kwa lengo la kuipa baraka.

Baada ya zoezi hilo kukamilika mfunguaji ambaye ni alikuwa katibu wa kamati ya  maandalizi ya harusi hiyo, aliitikisa na kuifungua kwa kutumia kifungulia chupa  cha kawaida (opena) ambapo ilifoka na kumwagika kama Shampeni.

Alipohojiwa na mwandishi wetu kuhusiana na tukio hilo, alisema wao kama walokole hawatumii kinywaji chochote kinachoshabihiana na kilevi.

"Tunajua fika kuna Shampeni zisizokuwa na kilevi lakini kwa kuwa ni jamii ya pombe, tumeamua kutovitumia, ndiyo maana unaona tunatumia soda kwenye sherehe zetu,” alisema katibu huyo.
Tukio hilo la Coca Cola linaonyeshwa katika picha zifuatazo: