Sudan Kusini latangazwa kuwa taifa la 54 la bara la Afrika
HONGERA SANA SUDAN
Sudan Kusini yasheherekea uhuru
Jamhuri ya Sudan Kusini kwa sasa inashereheklea uhuru wake baada ya kutangazwa rasmi kuwa taifa huru la 54 la bara la Afrika uhuru ambao umepatakina baada ya vita vya miongo kadha. Kulikuwa na mbwembwe na vigelegele kwenye mitaa ya mji wa Juba huku wenyeji wa taifa la Sudan Kusini wa wakipeperusha bendera ya taifa lao jipya. Viongozi kutoka sehemu mbali mbali za ulimwengu walihudhuria sherehe hizo akiwemo rais Omar al-Bashir akisimama na rais wa Sudan Kusini Salva Kiir, ukiwemo pia ujumbe kutoka Umoja wa Mataifa ukiongozwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon. Ban amesema kwamba leo tunashuhudia historia ya kuzaliwa kwa nchi hii jipya.
SAUTI YA KATIBU MKUAA
Na pia Ban aliwaambia watu wa Sudan Kusini:
“Hii ni lazima iwe siku ya hisia na raha kwa watu wote wa Sudan Kusini, lakini pia hii ina maana kwa nchi zote za eneo hili. Mmetoka mbali lakini uhuru utakuwa ni mwanzo tu. Ni lazima muifanye nchi yenu kuwa nchi ya maendeleo na yenye imekomaa kidemokrasia. Hii ndiyo ahadi ya Umoja wa Mataifa ya kuwasaidia. Niko hapa kuonyesha uungwaji mkono wangu na wa Umoja wa Mataifa kwa watu wote hapa.”
Umati uliohudhuria sherehe hizo chini ya jua kali ulishangilia wakati bendera ya Sudan ilipoteremshwa na bendera mpya ya taifa la Sudan Kusini kupandishwa na tarumbeta kupiga wimbo mpya wa taifa
Kifaa hiki hakikutengenezwa kwa ajili ya kumilikiwa na watu weupe tu. ila mpaka sisi. kwani tunazana kali zaidi ya hao watu weusi licha ya kwamba tunatumia slaa zao. na bora upigwe na risasi ya mguu kulioko mshale.. yaaani unaingia utafikiri tonge na ugali na mlenda.. rahaa kweli.. ila haikutengenezwa kwa ajili ya kuua watu wasiokuwa na hatia laghasha ni kwa wale wanaovunja hamri kumi za mungu na za nchi yeyote Duniani..
Baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Nawenge, Tarafa ya Vigoi, Wilaya ya Ulanga, wakijitolea kufyatua tofali kwa ajili ya shughuli za ujenzi wa vyumba vya madarasa ya shule za msingi, sekondari, zahanati na vituo vya Polisi, katika tarafa hiyo kama walivyokutwa kijijini hapo.
Geofrey Nyang’oro, Dar na Leo Bahati, Dodoma
SIKU moja baada ya Serikali kumkingia kifua Mbunge wa Bariadi Mashariki (CCM), Andrew Chenge ili asishtakiwe kwa rushwa katika mchakato wa ununuzi ya rada, Chadema imeweka hadharani kurasa 11 za ushahidi inaodai kuwa unaweza kumtia hatiani Mwanasheria Mkuu huyo wa zamani wa Serikali kama atashtakiwa.Ushahidi huo uliotolewa jana na Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa, ni ripoti ya uchunguzi uliofanywa na Shirika la Upelelezi la Makosa Makubwa ya Jinai la Nchini Uingereza (SFO)
VURUGU YA KUGOMBEA MAITI: POLISI POST, MSIKITI VYAPIGWA MAWE JIJINI DAR
Vurugu ya kugombea maiti imezuka jioni hii eneo la Manzese Tip Top na kusababisha uharibifu wa mali na majeraha kwa waandishi wa habari waliokuwa wakifutailia sakata hilo. Mwandishi wa mtandao huu anapasha kuwa ugomvi huo umezuka baada ya kijana mmoja kufariki katika mazingira ya kutatanisha, kundi moja la familia liliamua kuzika lakini likaibuka kundi la pili kuzuia kuzika maiti hiyo iliyokwisha pelekwa msikitini kwa kuombewa kabla ya kuzika. Kundili hilo lilipiga mawe msikitini na hata polisi walipoingilia kati nao walipigwa mawe, furugu zikaendelea hadi kituo cha polisi Mabibo Mpakani na Manzese Midizini ambako vimeharibiwa kwa mawe. Pikipiki ilichomwa moto, msikiti wa Tawfiq Manzese (pichani chini) nao ulipigwa mawe.
Pichani juu ni mwandishi wa gazeti la Sani Christopher Lissa akiwa na jeraha alilolipata katika vurugu hizo na picha nyingine inaonesha jinsi 'kaunta' ya kituo cha polisi ilivyoharibiwa.
HAYA NDIYO MAMBO YALIYOTOKEA HUKO MWANZA. BAINA YA MACHINGA NA POLISI.
machinga
Kijana akikimbia na televisheni anayodaiwa kupora katika duka la Zara Solar Limited lililopo Barabara ya Nyerere jijini Mwanza baada kutokea vurugu za wamachinga na polisi jana.(Picha: Cosmas Mlekani)
. Wengi wajeruhiwa kwa risasi za moto, wawili wako hoi ICU
.Yachomwa, maduka yavunjwa, ngawira zaporwa
Milio ya risasi, mabomu ya kutoa machozi ilitawala Jiji la Mwanza wakati Polisi walipopambana na wafanyabiashara ndogo ndogo maarufu kwa jina la wamachinga, walioasi wakikataa kufukuzwa katika mitaa ya jiji hilo kufanya uchuuzi.
TANZANIA SI MASIKI ILA WATANZANIA NDIO MASIKINI!!!
kundi la nyani
Tanzanite
Almasi/diamond
Dhahabu/gold
mlima kilimanjaro/mount kilimanjaro
Kutokana mwangajamii kufanya uchunguzi imegundua asilimia kubwa ya watanzania, wanajua nchi yao ni masikini.. lakini hapana ila watanzania ndio masikini. nasema hivyo nikiwa na maana kuwa ni mfumo 2 fulani ndio unaosababisha mtanzania kuwa na umasikini. ikiwemo uwongozi uliotawala sekta za uchumi. kushindwa kusimamia utajiri ulipo ndani ya tanzania na hatimae wanaofaidi ni watu kutoka nje.na ukichunguza sana ajira nyingi sana watanzania wapo kwa 60%peke yake ndio maana mpaka leo ukifanikiwa kuajiriwa na mtanzania mwenzio cha moto utakipata. maana utatumishwa na kama punda lakini cha ajabu mtu kutoka nje.. utaona atakavyotukuzwa hata mungu siyo hivyo. mali ya sili ya tanzania ingepata mtu makini basi, tanzania inuwezo wa kulisha africa mashariki nzima..
NINI KIFANYIKE ILI KUONDOKANA NA UKATILI WA KIJINSIA MAJUMBANI?
UKATILI WA MAJUMBANI
Utangulizi
Ukatili wa majumbani ni aina ya tabia inayotumika kujenga uwezo wa mtu mmoja kummiliki mwingine kwa kutumia vitisho na woga, ukatili wa majumbani aghalabu hutokea kwa watu walio na uhusiano wa kimapenzi na hata wale wanaoishi nyumba moja
Magomvi ya nyumbani pamoja na mambo mengine huhusisha kipigo cha wazi au cha kisiri, kuitana majina yasiyofaa, kutumia fedha kwa madhumuni ya kumiliki wengine, kutumia lugha ya matusi, kubaka watoto ndani ya nyumba, kuwamiliki watoto, kutenga na kutumia vitisho.
Aina za ugomvi
Kipigo
Kusukuma, kupiga, kuburuza, kukanyaga, kukaba, ngumi, kuunguzwa, kuvunjwa mikono, kupigishwa kichwa ukutani au sakafuni, na kutumia nyenzo yoyote kama silaha
Emotional/athari za kihisia au kiakili
Kupiga kelele, kuapiza, kuvunja utu, kuaibisha, kukosoa, kulaumu, kutishia kudhuru, kufungiwa nje ya nyumba, kutishia kuondoka, kushikashika simu ya mwenzio!!!!!!!!.
Kujamiiana
Kubaka/ubakaji ndani ya ndoa, kushikwashikwa kimwili bila ridhaa, kufanya mapenzi kinyume cha maumbile asilia/ridhaa, kutumia nguvu, kujamiiana kwa kukomoa, kutokuwa mwaminifu na ndoa yako, kuingiza vitu sehemu za siri, kukataa kujamiiana kwa salama.
Kiuchumi
Kuzuia hela za familia, kumkataza mwenza kufanya kazi,kumfanya mwenzio awe anaomba fedha za matumizi na au kumpatia kwa masimango, kuomba mshahara wa mwenzio, kutomruhusu mke kuwa na fedha, kutumia mali/fedha za familia bila ridha ya mwingine, kutomruhusu mke kumiliki mali.
Tamko la Kimataifa la Kuondoa Vitendo viovu dhidi ya Wanawake la 1993 linafasiri ukatili wa kijinsia kama kitendo chochote kile ambacho matokeo yake yanamfanya mwanamke aumie kimwili, kisaikolojia na kimapenzi iwe kwa mtu binafsi au kwa umma[1].
Unyanyasaji kijinsia nchini Tanzania bado ni mkubwa kwani mwaka 2007, jumla ya matukio 6,531 ya vitendo vya unyanyasaji kijinsia yalitokea[2]
Ukatili baina ya wanandoa na wasio wanandoa umekithiri sana katika miaka ya karibuni, mwezi Novemba 2007 zilitolewa taarifa kwamba asilimia 50 ya wanawake Tanzania hupigwa kila siku kutoka kwa wenzi wao[3].mbali na hapo katika utafiti uliofanyika mwaka 2006, asilimia 25 ya wanawake waliohojiwa walikiri kufanyiwa ukatili kwa wapenzi wao wasio wanandoa[4] utafiti ambao ni sambamba na ule ulioonyesha kwamba 1 kati ya wanawake 10 amefanyiwa ukatili katika umri wa miaka 15 na mtu asiye mpenzi wake.
ukatili wa kimwili katika ndoa na kwa wapenzi husababisha majeraha madogo ambayo hatimaye hukua na kuwa makubwa, shirika la afya duniania lilifanya utafiti na kubaini kuwa asilimia 30 ya wahanga wa ukatili huu hupata majeraha makubwa baada ya kupigwa vibaya[5]
Sababu kubwa ya ukatili huu dhidi ya wanawake ni kuwepo kwa mila na desturi ambazo zinalea ushambuliaji na unyanyasaji wa wanawake[6]. Ambapo vitendo hivi hushamiri na kukomaa na hatimaye kuwa kama sehemu ya maisha ya kawaida, upo ushahidi kuwa katika baadhi ya makabila hapa nchini mwanamke kutokupigwa ni ishara mbaya kwamba mumewe hana wivu naye. katika utafiti uliofanyika mwaka 2006, asilimia 60 ya wanawake waliohojiwa walisema kwamba wanaamini mwanamke kupigwa ni jambo la kawaida[7] tatizo hili ni kubwa kwani ni moja ya changamoto katika kupinga aina hii ya ukatili, changamoto nyingine ni pamoja na kushindwa kutoa taarifa na pia kutokana na shinikizo la jamii au familia kutaka kumaliza mambo kiungwana, wanawake wengine wamearifiwa kufumbia macho ukatili huu ili kunusuaru watoto na au ndoa zao[8] aidha kuogopa waume zao kupelekwa jela iwapo taarifa zitafika kwa vyombo vya dola na waume hao kuchukuliwa hatua za kisheria[9]
Serikali ya Tanzania imekuwa katika juhudi mbalimbali za kutokomeza ukatili wa majumbani, Mwaka 2001 Serikali ya Tanzania ilizindua Mpango wa Taifa wa Kupinga Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto (2001-2015). Hata hivyo mpango huu umekuwa ukisuasua utekelezaji wake kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ya ukosefu wa fedha na mfumo wa msaada wa kisheria ambapo mwanamke mhanga wa ukatili anaweza kuupata. Mwezi Mei 2008, serikali ilichukua hatua nyingine ya kutafuta suluhu ya tatizo la ukatili wa majumbani kwa wanawake kwa kupitisha mfuko Maendeleo wa Umoja wa Mataifa wa Kampeni ya kupinga ukatili dhidi ya wanawake[10], serikali pia imetoa msukumo kwa wanawake kujitokeza kusema hapana dhidi ya ukatili wa majumbani ili kulinda haki zao[11]
hata hivyo kuna makosa mengi ndani ya sheria ya Kanuni za Makosa ya Jinai ambayo hayamlindi mwanamke kikamilifu dhidi ya unyanyasaji kijinsia mfano katika kosa la kubaka ambapo linatumika kwa watu wasiokuwa katika ndoa tu au waliotengana[12], sheria hii imekaa kimya kuhusu ubakaji ndani ya ndoa.
Kuhusu kampeni ya Tunaweza;
Kampeni ya Tunaweza ni kampeni kubwa inayoendelea kidunia ambayo lengo lake kuu ni tukokomeza ukatili dhidi ya Wanawake, na katika ukanda huu wa Afrika Mashariki, kampeni hii imeenea zaidi kwa Tanzania na Kenya kutokana na ukweli kwamba kuna utamaduni wa ukimya na kufumbia macho ukatili huu miongoni mwa jamii. Kampeni hii ina lengo la kupata wigo mpana wa ushiriki wa jamii iliyo tayari (critical mass) katika kuzuia ukatili dhidi ya wanawake hasa ukatili wa majumbani na ambao pia watakuwa ni chachu ya mabadiliko katika jamii, katika mashirika na taasisi kufikia mwaka 2012
Malengo mahsusi ya kampeni hii ni;
Kufanya mageuzi katika imani na desturi katika jamii zinazochagiza ukatili dhidi ya wanawake
Kutanua wigo ushiriki mpana wa jamii kusimama kidete na kwa pamoja katika kupinga ukatili dhidi ya Wanawake
Kuanzisha vuguvugu la jamii kupinga ukatili dhidi ya wanawake
Kuunda mitandao ya kitaifa na kikanda katika kupinga ukatili dhidi ya wanawake
Mikakati ya Kampeni ya Tunaweza;
Kuhamasisha waleta mabadiliko 1.6 milioni katika Tanzania
Mleta Mabadiliko ni mtu yeyote anayehiari na anayethubutu
ØKuadilika kitabia kuachana au kupamban ukatili dhidi ya wanawake