May 20, 2011

Israili yapinga pendekezo la Rais Obama Benjamin Netanyahu

Benjamin Netanyahu
Waziri Mkuu wa Israili Benjamin Netanyahu.
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amepinga pendekezo la rais wa Marekani Barack Obama kuwa Jamhuri ya Palestina lazima iundwe kuzingatia mipaka iliyochorwa mwaka wa 1967.
Katika hotuba muhimu ya serikali ya Marekani, Bw Obama amesema ''makubaliano ya kubadilisha mipaka kwa haraka'' yatasaidia kuunda Palestina salama .
Lakini Bw Netanyahu amesema mipaka hiyo, ambayo ilikuwepo kabla ya vita vya 1967, katika Mashariki ya kati hayawezi kulindwa.
Bw Netanyahu amajiandaa kukutana na Bw Obama kwa mazungumzo katika Ikulu ya White House.
Takriban raia wa Israel 300,000 wanaishi katika makazi waliojenga katika ukingo wa magharibi mwa mto Jordon, ambayo yako nje ya mipaka hiyo.
Makazi hayo yamejengwa kinyume na sheria za kimataifa, japo Israel inapinga hilo.
Katika hotuba yake, ya sera za Marekani katika Mashariki ya Kati, Rais Obama amesema msingi wa mazungumzo ya amani ni kuunda Palestina mpya na yenye salama.
Bw Obama amesema, ''Marekani inaamini kuwa matokeo ya mashauriano yanapaswa kuwa nchi mbili, huku Palestina ikiwa na mipaka ya kudumu kati yake na Israel, Jordon na Misri''.

May 18, 2011

VIONGOZI WA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TZ MBONA HAMUELEWEKI?

SHIRIKA  LA  UMEME TANESCO   NA  SHIRIKA  LA  MAJI SAFI  NA  MAJI TAKA  DAWASCO  MBONA   MMEKUWA  KERO  TANZANIA.? TANZANIA  MPAKA  SASA   HAINA  MAJI  SAFI... UMEME  WA  KUAMINIKA.  KWA  KUWA  SERIKALI  YENYEWE  HAINA    MUELEKEO  WA  MAENDELEO.  BAADHI  YA  VIONGOZI    WANAWEKA    FEDHA  ZA  WANANCHI   MIFUKONI  MWAO  NA  KUJILIMBIKIZIA  MALI....  NA  NDIO  MAANA    HATA  WAWEKEZAJI  HAWARUHUSIWI   KUWEKEZA...  NA    MUEKEZAJI  ATAKAE  WEKEZA  TANZANIA  LAZIMA  AWE  FISADI...  INASIKITISHA  SANA  KWA  MTANZANIA    KULALAMIKA  UMASIKINI  NA  WAKATI  VIONGOZI...  WAKIJILIMBIKIZIA  MALI  HUKU  MTANZANIA   AKITESEKA  KWA   UMASIKINI..  SASA  HIVI  VIONGOZI  WETU   WAKISHINDANA  KWA  MISHAHARA.....  LEO  HII  MTANZANIA  UNAPANDISHIWA..GHARAMA ZA MAJI, UMEME, CHAKULA  NK.   NI KUTOKANA  NA  WALAFI  WALIOPO   SERIKALINI..  HII  INACHUKUA  SURA  KUWA  NCHI  YETU  INAELEKEA    KUBAYA.....NAWEZA  KUSEMA  TANZANIA  VIONGOZI  WALIOBAKI  WAZALENDO  NI 5%  KUTOKA  100%    JE  NCHI  HII  ITAPONA  KWA  HAWA  MAFISADI?  SASA JIULIZE  KAMA  MTANZANIA  KODI ZOTE  ZA  WANANCHI   ZINAKWENDA  WAPI?
MF:
GHARAMA  ZA  UMEME  NA  MAJI  ZIMEKUWA  JUU,  NA   MAJI  VIVYO HIVYO..  HUKU TRA  WAKICHUKUA  KODI  MBALIMBALI.  SASA  HIZO  FEDHA  ZINAKWENDA  WAPI?

NDUGU  MTANZANIA  MPAKA  SASA  UMEJIPANGA  VIPI?

JAMANI WATAALAM WA KUJINYONGA MPO? SOMA HABARI HII YA KUTISHA. KISHA TOA MAONI NA MTAZAMO WAKO.


Mchungaji wa kanisa moja huko California Marekani, Harold Camping, ametabiri kuwa Mei 21,2011 saa moja kamili usiku mwisho wa dunia, na huenda tusiione tena jumapili ya wiki ijayo, kwani dunia itakuwa imefika mwisho  wake siku hiyo ya Jumamosi.

Mchungaji Camping kwa kutumia mahesabu ya tarehe na mafunzo ya Biblia, ametabiri kuwa kiama kitakuwa jumamosi, na miezi mitano baadae kwenye tarehe 21 Oktoba, Mungu ataiteketeza dunia.

 Mchungaji Camping ambaye anamiliki radio ya Christian Family Network yenye mtandao mkubwa sana nchini humo na sehemu zingine duniani ikiwa inarusha matangazo kwa lugha zaidi 48 zikiwemo lugha kutoka Afrika Kusini.
Camping mwenye umri wa miaka 89 ana wafuasi wengi sana duniani na sasa anaendesha kampeni kubwa kuwajulisha watu kuhusu mwisho wa dunia hapo Mei 21.







agari yenye mabango yenye ujumbe mwisho wa dunia Mei 21 yamekuwa yakionekana sehemu mbalimbali za Marekani yakitangaza kuwa mwisho wa dunia ni Mei 21 kwa sababu itakuwa ni siku ya 722 500 tangu Yesu aliposulubiwa msalabani mnamo Aprili moja AD33.
Aidha  Mchungaji Camping amesisitiza kuwa kuwa namba 722 500 ni muhimu sana kwa wakristo duniani kwani inapatikana kwa kuzizidisha namba tatu tukufu (5, 10, 17) mara mbili {5x10x17x5x10x17}

Hii sio mara ya kwanza kwa mchungaji Camping kutabiri matukio makubwa duniani coz Septemba 6 mwaka 1994 akiwa na wafuasi wake wengi walikusanyika mbele ya ukumbi wa Alameda wakisubiri kurudi kwa Yesu Kristo ambaye hakutokea na tangu wakati huo,camping amesema kuwa wamefanya utafiti mkubwa sana na hivyo wana uhakika safari hii utabiri wao utakuwa sahihi.

Kwa habari zaidi bonyeza hapa>>>>> 

May 16, 2011

Jua haki yako unapokamatwa na polisi.

  • Raia ana haki ya kumwomba askari ajitambulishe kwako.
    • Mwulize jina lake
    • Mwulize namba yake ya uaskari
  • Raia ana haki ya kujulishwa kwanini anatiliwa mashaka ama kukamatwa.
  • Raia ana haki ya kuwajulisha ndugu, jamaa ama sehemu anakofanyia kazi kwamba ama amekamatwa na polisi ama Taasisi ya Kuzuia Rushwa.
  • Raia ana haki ya kuomba na kupewa dhamana wakati akiwa kituo cha polisi ama Taasisi ya kuzuia rushwa.
    • Hutakiwi kutoa fedha kama dhamana uwapo kituo cha polisi ama Taasisi ya Kuzuia Rushwa, isipokuwa maelezo utakayoandika.
  • Raia ana haki ya kuwaeleza polisi ama Maafisa wa Kuzuia Rushwa kwamba lolote atakalosema linaweza kutumiwa kama ushahidi mahakamani, na asiburuzwe kuandika tu.
  • Raia ana haki ya kuomba Wakili wake awepo kituo cha polisi ama Taasisi ya Kuzuia Rushwa wakati anatoa maelezo yake.
  • Raia ana haki ya kuyasoma kabla ya kutia sahihi yake.
  • Raia ana haki ya kudai risiti ya orodha ya vitu vyake/fedha zake alizozitoa ama kukabidhi kituo cha polisi ama Taasisi ya Kuzuia Rushwa.
  • Raia kama ni mwanamke ana haki ya kupekuliwa na polisi wa kike, na iwapo hakuna polisi mwanamke, basi mwanamke yeyote na vile vile kwa mwanamume.
  • Raia ana haki ya kufikishwa mahakamani katika muda usiozidi saa 24 tangu alipokamatwa na kufikishwa kituo cha polisi.

WAZEE WA KATIBA MPYA MPO NA JAZBA ZENU?

Inaelekea siku hizi ili kuthibitisha msimamo wako ni lazima ukasirike, uanzishe vurumai, na kupandisha mori.

Siasa zetu siku hizi zimekuwa za kuchochea hasira na munkari usioeleweka mwanzo wake. Wenye dhamana ya kutuliza mori nao hupandisha mori, mitaani hakukaliki wala hakulaliki.
Siku hizi wenye kukunja nyuso zao kwa jazba ambazo huumba mistari mithiri ya upinde wa mvua wanaelekea kuteka jamii ati kwamba wajuvi.

Watu wanadhani kuwa tabia za ubedui ndiyo inadhihirisha kwamba wewe ni jogoo unayeyajua kuliko wale waliokaa kimya ama wanaofuata taratibu madhubuti kwa suala husika.

Ugangwe ni mzuri kwa mwenye busara, lakini siyo kila kitu kinahitaji uwe gangwe ndiyo ueleweke. Inawezekana ukawa mwehu kudai kitu mithiri ya mwehu, lakini wehu huo una busara zake ambazo unakuondoa katika jopo la wehu halisi mitaani.

Sote tunatambua katiba ni mali yetu na ndiyo inayojenga msingi wa nchi yetu. Tunajua kuwa kila katiba inapohitaji marekebisho ama kubadilishwa zipo taratibu za kufuatwa ndiyo maana tumeona Mbunge wa jimbo la Ubungo kwa tiketi ya chama cha demokrasia na maendeleo (chadema), John Mnyika amewasilisha hoja yake rasimu ya katiba mpya kwa katibu wa bunge la jamhuri ya muungano.

Mbunge John Mnyika amefuata taratibu wala hajapandisha mori kuonyesha anahamu sana na katiba mpya.
Hii ni busara na taratibu zinazopendeza watu wote. Na hamu yake inakuwa katika utaratibu wenye uchochezi kifikra kwakuwa tayari ameueleza katika njia halali.

Ndiyo, tunajua kuwa madai ya katiba mpya siyo mageni na hayataisha leo kwakuwa jamii inabadilika na kila mmoja anapenda kujipendelea kwa lolote lililopo.

Kila mmoja anatambua haki ya kuwa huru na kufanya mambo bila kuvunja katiba. Kila mmoja anaweza kushiriki siasa, lakini hakuna maana ushiriki huo uambatane na ngumi ama mateke.
Kwamba kufanya hivyo ndiyo unadhihirisha umwamba wa madai yako. Dai haki yako kwa utaratibu unaoleweka.

Dai katiba mpya ukitofautisha na kudai kitumbua cha chai ulichodhulumiwa nyumbani.
Kulinganisha madai ya katiba mpya na kudai andazi nyumbani ni mantiki iliyopinda. Kudhani maguvu yanaweza kuzalisha katiba mpya mimi naamini tunakosa uelewa juu ya kusimamia madai.

Usilinganishe kudai kalamu ya wino uliyoibiwa shule na suala la katiba mpya.
Kama mkeo anavuruga bajeti ya nyumba basi panga njia halali ya kudai mabadiliko, kumzaba ngumi na mateke haisaidii kitu. Ni sawa na dai hili la katiba, tuidai kwa adabu hata kama ni laiki yetu.

Hili ni sawa suala linalojitokeza sasa kuwa kudai katiba mpya ni lazima watu kuanza kutoana ngeu. Huu ni utaratibu wa kihuni, tunataka njia muafaka ya kuwasilisha madai yako.
Sidhani kama huyo mwendesha mashtaka wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu Luis Moreno Ocampo anaweza kuruhusu kupokea madai ya katiba mpya Tanzania kwa kutishwa kung’olewa meno. Hatuhitaji ngumi wala mateke.

Watu wenye akili zao, na wenye kuelewa kabisa utaratibu wa kudai katiba mpya wanaamua kuanzisha zogo la kutoana ngeu na kung’oana meno.
Hili siyo jambo zuri, maana tunajua kila zuri lina dosari zake. Nimebahatika kuisoma na kuzielewa katiba zote mbili yaani ya Jamhuri ya Muungano na katiba ya Zanzibar.

Nakiri ipo dosari ambazo nachelea kuainisha kwakuwa siyo mtaalamu wa sheria. Lakini ipo dosari moja rahisi mno ilifanyika mwaka 1994 ya kuondoa kipengere cha makamu wa kwanza wa rais wa Jamhuri ya Muungano ambaye alikuwa pia rais wa Zanzibar.

Kwa maoni yangu hatukupaswa kukiondoa kipengere hicho kwakuwa kinaonesha umuhimu mkubwa sana wa kuuthamini muungano wetu. Kuondolewa kipengere hicho kinadhorotosha muungano wetu na mshikamano uliopo.

Pamoja na dosari hizo kujitokeza, lakini bado sijaona sababu ya kudai katiba mpya kwa msingi wa mangumi na mateke.
Tumeona wafuasi wa chama cha wananchi (CUF) wakiandamana kudai katiba, tumeona mikogo mingi na harara za kudai katiba mpya inashamiri.

Mikusanyiko na mijadala juu ya katiba mpya inafanyika kwa kutazamana usoni, kama hujashiriki katika kampeni ya kudai katiba kwa munkari basi unacharazwa mangumi na mateke.

Sijui huu ni utamaduni wa aina gani, na sijui kwamba ukiwa na hasira zako juu ya katiba mpya ndiyo utaeleweka sana au la.
Maandamano haya yamekuwa wakiwafanya Polisi wawe makini na uendeshaji wake. Natambua kwamba suala la katiba ni letu sote na linaihusu nchi yetu.

Lakini hakuna sababu ya msingi kutwangana makonde na kuchaniana mashati kwasababu ya kudai katiba. Sote tunahitaji kujenga hekalu moja, hivyo, basi tubomoe mlango huo kwa hekima.

Tunaruhusu Polisi kuvurumisha mabomu ili kutuliza jazba za waandamanaji wa kudai katiba mpya wakati hakuna sababu yeyote ya kudai katiba kwa mijeledi.

Utamaduni wa kudai kila kitu kwa mikwaruzano unashamiri, wapo wenye madai ya msingi lakini namna uwasilishaji wa vilio vyao na kwakutumia ngumi, mateke na mikwaju wanadhani wataeleweka.

Narudia tusiige utamaduni wa ngumi na mateke kufanikisha azma zetu. Kati ya waandamanaji hawa ukiuliza unaijua katiba hiyo unayoikashifu, hana jawabu.

Je unaifahamu kiasi gani katiba inayoongoza nchi hii na ambayo unaambiwa ina viraka? Hakuna mwenye jawabu bora labda kwa wale waliofanikiwa kuzisoma na kuelewa.

Hata hivyo makundi ya waandamanaji wengine wa kudai katiba hususani yaliyofanywa na CUF wapo watoto wadogo waliojiingiza katika maandamano hayo. Sina mashaka walikuwa wanafunzi.

Hawa tunawafundishi njia ya kudai haki(?) ni kwa maandamano, utamaduni huu ukimea unazaa taifa la waandamanaji. Tunawajuza kudai haki kwa kupigana makonde, kutoana ngeu na kadhalika.

Dhima ya kudai haki ni kuhitaji mabadiliko kwa mujibu wa nyakati zetu na zijazo lakini ni muhimu kuelewa kuwa azima ya kudai haki ni kuweka mambo sawa. Kwahiyo usawa huu unapaswa kuenenda utaratibu unaoeleweka.

Vuguvugu la kudai katiba halimaanishi nyote mkunje ngumi na kurusha kwa wengine au kuwatoa mkuku wengine ili washiriki madai haya. Kila mmoja anapima kwa nafasi yake, anachanganua,anaafiki kuwa madai haya ni halali.

Na anayasimami kwa uhalali wala havurumishi ngumi au teke kwa mdaiwa. Bali simamieni hoja kwa utulivu, tuepuke tabia za amri. Na katiba yetu inakuja kwa namna tutakavyotaka. Amani iwe kwenu nyote

May 15, 2011

UCHUNGUZI ULIOFANYIKA KUHUSU MAGARI USED.

INASEMAKANA    NCHI  INAYOONGOZA   KWA  KUNUNUA  MAGARI  USED  DUNIANI  KUTOKA  JAPANI  NI  TANZANIA.  KWANI  WATANZANIA  WENGI  HALI  ZA  KIFEDHA   ZIKO  CHINI  SANA.  KWA  KWA  1.5 % NDIO  WENYE  UWEZO    WA  KUNUNUA  MAGARI  NEW  NA  ASILIMIA  ILIYOBAKI   WANANUNUA  TU  USED  CAR  KUTOKANA    NI  KIPATO  CHAO  KUWA   KIDOGO.  NA  MKOA  WENYEWE  UNAONGOZA  KUWA  NA  MAGARI    MABOVU    TANZANIAN   NI  DAR  ES SALAAM.  SASA  TANZANIA  INABIDI   KAMA  TANZANIA  IANGLIE  HALI    YA  WATANZANIA     WALIOKUWA  HALI  YA  CHINI  NA  HALI  YA  KATI.  NJIA  MUHIMU  NI  KUIMARISHA   HALI  YA  UCHUMI  NA  RASILIMALI ZA  NCHI  YETU.  TUJIANGALIE  YA  RASILIMALI  ZETU  NA  SI  KFAIDISHA  WENGINE  AU  WAEKEZAJI.