May 07, 2011

Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein akifuatana na Makamu wa Kwanza wa Rais, Maalim Seif Sharif Hamadi.

Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein akifuatana na Makamu wa Kwanza wa Rais, Maalim Seif Sharif Hamadi wakati wa mapumziko ya mkutano wa kuimarisha uhusiano baina ya viongozi wa kisiasa na kiutendaji serikalini unaoendelea katika Ukumbi wa Zanzibar Beach Resort, Zanzibar.

May 03, 2011

LIBYA

Historia ya Gaddafi

Kanali Muammar Gaddafi ni kiongozi aliyekaa madarakani kwa muda mrefu zaidi barani Afrika na katika nchi za Kiarabu.
Gaddafi
Gaddafi
Ameongoza Libya tangu alipompindua Mfalme Idris I, katika mapinduzi yasiyo ya kumwaga damu, wakati huo akiwa na umri wa miaka 27.
Maarufu kwa nguo anazopenda kuvaa, na walinzi wa kike wenye kubeba silaha, kiongozi huyo wa Libya pia anadhaniwa kuwa na mbinu nzuri za kisiasa, kwa kuweza kuirejesha Libya kutokana na kutengwa kidiplomasia duniani.
Baada ya miongo miwili ya kutengwa katika jamii ya kimataifa, mwaka 2003, Tripoli ilikiri kuwa walifanya shambulio la Lockerbie kwa kuiangamiza kwa mabomu ndege ya Pam Am na hapo Umoja wa Mataifa ukaondoa vikwazo dhidi ya Libya.
Gaddafi mwaka 1969
Gaddafi mwaka 1969
Baada ya miezi kadhaa, serikali ya Kanali Gaddafi ilisitisha mipango yake ya kuunda silaha za maangamizi na hii ikarejesha ushirikiano na nchi za magharibi.
Hapo ndipo mabadiliko halisi yalionekana kwa kuwa nchi hizo za magharibi zilibadili mtazamo wao na kuacha kumtenga Gaddafi na kushirikiana naye hata kama alikuwa hatabiriki.
Ni mtu wa kipekee katika kauli zake, mienendo yake, tabia zake na mikakati yake, kwa mujibu wa Saas Djebbar mtaalam wa siasa za Libya.
'Lakini ni mwanasiasa mashuhuri; hakuna shaka lolote kuhusu hilo. Ni mwanasiasa anayeweza kuhimili misukosuko ya kisiasa kwa hali ya juu sana.'

Asili ya Mabedui

Muammar Gaddafi alizaliwa jangwani karibu na Sirte mwaka 1942.
Gaddafi katika mkutano Sirte
Gaddafi katika mkutano Sirte
Alipokuwa kijana alivutiwa na kiongozi mzalendo wa Misri na, Gamal Abdel Nasser, alipokuwa akishiriki katika maandamano dhidi ya Israel wakati wa mtafaruku wa Suez mwaka 1956.
Gaddafi alipanga njama ya kupindua utawala wa kifalme alipokuwa mwanafunzi wa kijeshi na aliwahi kupata mafunzo zaidi akiwa Uingereza kabla ya kurejea nyumbani Libya, mji wa Benghazi, na kupanga mapinduzi ya tarehe 1 Septemba mwaka wa 1969.
Ghaddafi alianza kujenga itikadi zake za kisiasa mwaka 1970 na kuziandika katika kitabu chake cha kijani kibichi.
Gaddafi alipokuwa akizuru Senegal mwaka 1985
Gaddafi alipokuwa akizuru Senegal mwaka 1985
Alikitumia kitabu chake kuanzisha mfumo wa kisiasa iliyojumuisha kanuni za kiislamu na mfumo uliyo tofauti na siasa za ujamaa au ubepari.
Mwaka1977 aliasisi mfumo ujulikanao kama 'Jamahiriya' au 'Taifa la Umma' ambapo raia ndio wanaoendesha uongozi wa nchi yao kupitia 'kamati za umma'.
Hema ya Gaddafi
Hema ya Gaddafi
Mfumo huo wa Gaddafi umevuka mipaka na hauhusishi mambo ya siasa tu, bali pia mambo mengine.
Akiwa safarini ng'ambo, huwa anakaa kwenye kambi iliyojengwa na hema yake ya kifahari ya Kibeduwi akiwa amefuatana na walinzi wanawake ambao, inasemekana, huwa hawapotezi umakini kazini kama walinzi wanaume.
Hema hiyo pia hutumiwa kuwalaki wageni wa Libya na Kanali Gaddafi huendesha mikutano na mahojiano yake humo humo akipepea usinga au tawi la mitende.

Upekepeke

Benjamin Barber, mtaalam wa kisiasa wa kujitegemea, kutoka Marekani amewahi kukutana na Gaddafi mara kadhaa hivi karibuni na kuzungumza naye kuhusu mustakabali wa Libya.
Gaddafi akiwa na viongozi wengine wa nchi za Uarabuni
Gaddafi akiwa na viongozi wengine wa nchi za Uarabuni
Bw Barber alisema kuwa Muammar Gaddafi anajihisi kuwa msomi aliyebobea.
Muammar Gaddafi na Tony Blair waliwahi kuandaa mkutano wa viongozi kutoka nchi mbalimbali tarehe 29 Mei 2007 kwenye hema hiyo ya Kibedui.
"Utashangazwa kuwa ingawaje ni dikteta, ni mwanafalasafa na mwenye kutafakari jambo kabla ya kuzungumza," aliiambia BBC.
"Namchukulia sana kama mtu kutoka kabila la Waberber na mtu ambaye aliibuka kutoka tamaduni za watu wa jangwani, kutoka kwenye mchanga na kwa namna fulani kuna tofauti kubwa na uongozi wa kisasa, na kwa namna fulani hilo limemfanay awe mstahamilivu na mwenye msimamo."
Kanali Gaddafi amejitahidi kwa muda mrefu kutoa ushawishi wake nyumbani na ng'ambo.
Awali alituma jeshi lake nchini Chad ambapo wanajeshi walidhibiti ukanda wa Aozou, kaskazini mwa nchi hiyo, mwaka 1973.
Katika miaka ya 80 aliandaa mafunzo kwa makundi ya waasi kutoka Afrika Magharibi yaliyojumuisha wale wa Tuareg ambao ni Waberber.
Hivi karibuni aliongoza jitihada za kuwapatanisha waasi wa Tuareg kutoka nchi za Niger na Mali.

'Mbwa kichaa'

Jumuiya ya wanadiplomasia kuitenga Libya kulitokana na Kanali Muammar Gaddafi kuunga mkono makundi yeneye silaha, ikiwemo Irish Republican Army na Palestine Liberation Organisation.
Gaddafi akiwa na mwandishi wa habari wa BBC
Gaddafi akiwa na mwandishi wa habari wa BBC
Rais wa zamani wa Marekani Ronald Reagan alimwita Gaddafi 'mad dog' yaani 'mbwa kichaa' na Marekani ililipiza kisasi dhidi ya Libya kwa madai ya kuhusika na mashambulio ya anga barani Ulaya kwa kuvamia miji ya Tripoli na Benghazi mwaka 1986.
Ilisemekana kuwa Kanali Gaddafi alitikiswa na mashambulio ya mabomu hayo ambapo mtoto wake wa kike wa kufikia aliuawa.
Aliposhindwa katika jitihada zake za kuzipatanisha nchi za Uarabuni katika miaka ya 90, Kanali Gaddafi alielekeza nguvu zake barani Afrika na kupendekeza 'Muungano wa Nchi' za bara la Afrika.
Muuguzi wa Gaddafi
Muuguzi wa Gaddafi
Alianza kuvaa mavazi yake binafsi, sare za michezo zilizo na ngao za bara la Afrika au picha za viongozi kutoka bara hilo.
Wakati wa mabadiliko katika karne ya 20, huku Libya ikiwa inapata tabu kutokana na vikwazo dhidi ya nchi hiyo, alianza kurekebisha hali nchini mwake.
Mwaka wa 2003, mabadiliko yakaanza kuonekana na baada ya miaka mitano mkataba wa kulipa fidia kwa waathirika wa Lockerbire uliafikiwa na hii ikarejesha uhusiano kati ya Washington na Libya.
'Hakutakuwa na vita tena, mashambulio, na vitendo vya ugaidi' Kanali Gaddafi alisema alipokuwa akiiherehekea miaka 39 aliyokaa madarakani.

Changamoto za ndani


Kiongozi huyo wa Libya hujiona kama kiongozi wa kidini wa taifa hilo, akihakikisha kwa kile anachosema ni demokrasia.
Waandamanaji wa hivi karibuni Libya
Waandamanaji wa hivi karibuni Libya
Lakini katika hali halisi, wakosoaji wanasema Kanali Gaddafi amefanikiwa kudhibiti nchi hiyo.
Wanaompinga wamekandamizwa kikatili na vyombo vya habari vinabaki katika udhibiti mkubwa wa serikali.
Libya ina sheria ambazo haziwaruhusi watu kukusanyika katika misingi ya kisiasa zinazopinga mapinduzi ya Kanali Gaddafi.
Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch limesema serikali hiyo imewatia mbaroni mamia ya raia kwa kukiuka sheria hiyo na baadhi yao kuhukumiwa kifo.
Imeripotiwa kumekuwa na matukio ya utesaji na hata watu kupotea
Inadhaniwa kuwa Kanali Gaddafi anaandaa namna ya kukabidhi madaraka yake kwasababu ya umri aliyofikia sasa lakini haijulikani ni nani atakayerithi uongozi wa Libya kutoka kwa Gaddafi.
Sayf akiwa na ndugu yake Saad
Sayf akiwa na ndugu yake Saad
Kuna hisia kuwa mwanawe Sayf Al-Islam Gaddafi ndiye atarithi uongozi kutoka kwa baba yake na anaongoza katika kuleta mabadiliko.
Ingawaje Sayf ametangaza kuwa anastaafu siasa lakini kuna wanaohisi kuwa hii ni mbinu ya kuongeza ushawishi wake kisiasa.
Wakati huo huo, Gaddafi ameahidi kuwa wizara za nchi hiyo zitafutwa pamoja na bajeti zao
Utajiri utakaopatikana kutokana na mafuta utakabidhiwa moja kwa moja kwa wananchi.
Licha ya uchumi wa Libya kutoa fursa kwa wawekezaji wa nje, mabadiliko bado yanakwenda taratibu.
Waandamanaji wakichana picha ya Gaddafi
Waandamanaji wakichana picha ya Gaddafi
Walibya wengi wana wasiwasi juu ya mabadiliko yanayotokea na kuhisi kuwa hawapati manufaa kutoka rasilmali ya Libya, waangalizi wanasema kwani huduma za serikali ni duni pamoja na ubadhirifu mkubwa wa mali.
' Wanajihadhari sana katika mapambano hayo kwa kuwa hawataki mabadiliko yatakayolegeza nguvu za umma,' alisema Saad Djebbar
'Lakini wakati huo huo, Walibya wanafahamu kuwa wanahitaji kufanya mabadilko. Na ndio maana wanaenda taratibu sana.
Mfuasi wa Gaddafi
Mfuasi wa Gaddafi

May 02, 2011

Sasa matukio ya dunia

396_uhyn_ryby.jpg397_uhyn_ryb.jpg398_verliby.jpg399_uhyn_ptactva.jpg400_ryby.jpg

396_uhyn_ryby.jpgTangu mwisho wa mwaka jana, kuna siri kifo cha aina mbalimbali kote duniani. Kufa ghafla kwa idadi kubwa na bila sababu dhahiri. Sababu hiyo bado ni wengi hakuna athari. Nini sababu ya kifo kama mkubwa wa wanyama? Nini kinatokea kwa dunia yetu, hivyo huathiri utawala wanyama? Wanyama ni nyeti sana na athari mbalimbali kwamba mtu wala hata ilani ya shamba geomagnetic, kanda geopathic, ultra sound na zaidi. Kuzingatia yafuatayo utafiti wa wanasayansi Czech.
Ni madhara gani shamba magnetic ya wanyama?
wanasayansi Kicheki walikuwa na uwezo wa kuonyesha kuwa shamba magnetic, kwa mfano, chini ya nyaya high voltage ina athari demonstrable juu ya tabia ya wanyama. Wanasayansi alikuja mwaka jana na ugunduzi wa ajabu kwamba ng'ombe au mifugo ya kulungu na malisho kulungu wakati wa kulala na daima kurejea kwa miili yao ilikuwa ikisafiri kutoka kaskazini na kusini. Sasa inakuja timu na maarifa kwamba mchezo kupoteza uwezo wake wa chini ya mistari high voltage nguvu kutenda erratically kabisa, na inaendelea hadi wakati wa malisho na vyama mbalimbali vya kimataifa. Mara baada ya mchezo mbali na voltage ya juu, tena - wakati wa malisho au wakati wa kulala - kulinganisha ya mwili na mwelekeo wa kaskazini na kusini. "Madhara Kuingilia ya mashamba electromagnetic juu ya tabia ya mnyama ni kuzingatiwa mpaka futi hamsini kutoka mistari nguvu," anasema Pavel.
Wanasayansi kukubali kwamba ugunduzi wake kuufungua mlango wa chumba ambapo mtuhumiwa tu, yale yote inaweza kujificha. High voltage kuzuia ndani "compass" mchezo ". Chini ya nyaya hizo ndani vyema mchezo literally kufuta nje, hivyo ghafla kuanza kuishi tofauti Pavel Idara ya Wanyama, Chuo Kikuu cha Charles, alisema kuzuia asili" Compass "mchezo kama ifuatavyo:" The AC high voltage hutoa mchanganyiko magnetic shamba magnetism mabadiliko ya dunia, ambayo ni oriented kulingana na mifugo.
"Kama waya chini ya voltage high - na hivyo uwanja magnetic - uwindaji tofauti kuliko kawaida, ni hakika ina mabadiliko ya uzoefu wa ubongo, seli na Masi kiwango," anasema Profesa Hynek Burda wa Chuo Kikuu cha Duisburg-Essen. Matokeo ya ugunduzi wao latest inachapisha karibuni suala la jarida kifahari ya Marekani kisayansi Kesi ya Academy ya Taifa ya Sayansi. Chini ya makala ni saini na Profesa Burda, Sabine Begall, Pavel Nemec wa Chuo Kikuu na Charles Kicheki Jaroslav Cerveny Academy ya Sayansi.
Makala kamili hapa: idnes.cz
Je, vifo vya wanyama na baadhi ya uhusiano na kile kinachotokea kwa dunia yetu?
Mwaka 2004, ya kwanza katika historia ya cap ya barafu Arctic melted. Ya kudumu eneo waliohifadhiwa alianza fujo kutolewa methane kama vile kutoka seabed. Kudhoofisha Stream Ghuba juu yako, plankton haraka akifa msingi wa mzunguko wa chakula. Kuongezeka kuyumba kwa msingi wa dunia na kuongezeka kwa volkeno na tectonic shughuli. Katika anga ya juu ina gesi ambayo imekuwa huko mbele angalau. Ongezeko la matukio ya plasma anga mipira, mzunguko wa dunia katika kipindi cha miaka 20 ina sjunkit. Mwaka 1900 tulikuwa na kila aina ya wanyama milioni 30, sasa hivi ni chini ya nusu. Unaweza haya mabadiliko kwa joto duniani mtu,?
sayari yetu bila shaka ni kufa, wanyama ni kufa kwa kiasi kikubwa, ambayo ilitokea mapema. Ni kweli kwamba wanyama wanakufa kila molekuli, kama baadhi ya madai. Katika nusu tu ya miaka mia moja aina haiko na sasa kuanza mwishoni mwa mwaka jana kufuatia vifo wa unexplained wingi wa samaki na ndege wengi. Biblia inatuambia kwamba kwa sababu ya dhambi zetu, nchi itakuwa na nguvu, zikanyauka na fade. Hivyo, ni kweli hutokea.

NINI KIMEJIRI DUNIANI

OSAMA BIN LADEN AUAWA

Osama Bin Laden
Mwanzilishi na kiongozi wa kundi la kigaidi la Al Qaeda Osama Bin Laden ameuwawa na majeshi ya Marekani nchini Pakistan, rais Obama amesema.
Kiongozi huyo wa al-qaeda aliuwawa katika operesheni ya ardhini nje ya mji wa Islamabad kwa mujibu wa taarifa za kijasusi.
Bw Obama amasema baada ya ufyatulianaji wa risasi, majeshi ya Marekani ilichukua mwili wake.
Bin Laden anashutumiwa kwa kuhusika katika baadhi ya vitendo vya ukatili ikiwemo mashambulizi mjini New York na Washington, mnamo Septemba 11, 2001.
Kifo chake ni pigo kubwa kwa kundi la al-qaeda lakini kuelezea hofu kuwa huenda wakashambuliwa katika mashambulizi ya kulipiza kisasi.
Bw Obama anasema alielezea Agosti, mwaka uliopita, kuhusu kule Osama Bin Laden amejifisha. Kufuatia uchunguzi wa ujasusi waligundua amejificha mjini Pakistan.

Wiki iliyopita rais Obama alitoa amri kwa operesheni kufanyika ''kumsaka Bin Laden'' . Bw Obama amesema operesheni hiyo iliendeshwa na kundi ndogo la wanajeshi wa Marekani katika eneo la Abbottabad, Kaskazini mwa Islamabad.

''Baada ya ufyatulianaji wa risasi, Bin Laden aliuwawa na mwili wale kuchukuliwa na majeshi ya Marekani'' rais Barack Obama amesema. 
(habari  kutoka bbc)


                                                                                                                                                                  

HUKO LIBYA  TENA

Gaddafi anataka mazungumzo


Kiongozi wa Libya, Kanali Gaddafi, ametoa wito kwa Nato kwamba kufanywe mazungumzo ili kusimamisha mashambulio ya ndege za umoja huo dhidi ya nchi yake.


Katika hotuba iliyotangazwa kwenye televisheni, Kanali Gaddafi alisema yeye yuko tayari kusimamisha
 mapigano ikiwa itakubaliwa na pande zote.
Mlibya anatazama hotuba ya Kanali Gaddafi
Katika hotuba yake Jumamosi asubuhi, kiongozi wa Libya alisema yuko tayari kutoa amri kuwa mapigano yasitishwe na kuanza mazungumzo, endapo NATO itaacha mashambulio ya mabomu.
Lakini alikataa lile dai kubwa la wapiganaji na jumuiya ya kimataifa, kwamba yeye aondoke.
Alisema hatong'atuka wala kuihama Libya.
Wengi serikalini wanaona kuwa wameshakaribisha mazungumzo kwa kukubali mpago wa Umoja wa Afrika wa kurejesha amani; lakini wanahisi upinzani ndio hautaki kumaliza mapigano, kwa sababu unakataa kuzungumza na serikali ya Kanali Gaddafi.
Alipokuwa Kanali Gaddafi anazungumza, NATO ilidondosha makombora matatu mjini Tripoli, kwenye yale yaliyoonekana kama majengo ya serikali.
Hotuba ya Kanali Gaddafi, ilikuwa mchanganyiko wa kukaza na kulegeza kamba.
Alisema kila mwananchi wa Libya sasa anakabili mambo mawili : uhuru ama kifo.
Hakuna kusalliam amri, hakuna hofu wala kuondoka.