
Boko Haram walitoa onyo la kufanya shambulio
 Shirika la Msalaba Mwekundu la Nigeria limesema watu sita wamekufa. Awali huduma za dharura zilisema watu 18 wameukufa.
Milipuko hiyo ambayo imesababisha uharibifu mkubwa, imetokea karibu na eneo lenye hoteli nyingi na kanisa moja.
                     Eneo hilo limekuwa likishuhudia mizozo ya kidini katika miaka ya hivi karibuni na kusababisha mamia ya vifo vya watu.
                     Kulikuwa na onyo lililotolewa kuhusu mashambulio hayo katika kipindi cha Pasaka.
                     Wengi wa waliokufa wanadhaniwa kuwa ni madereva wa pikipiki na kukodisha na omba omba wa mitaani.
                     Watu walioshuhudia wamesema vitu mbalimbali vilirushwa umbali mrefu kutoka katika eneo la tukio.
                     Hakuna yeyote aliyejitokeza kudai kuhuska na 
shambulio hilo, lakini mwandishi wa BBC nchini Nigeria Mark Lobel 
anasema kundi la wenye itikadi kali la Boko Haram lilisema kuwa 
lingefanya mashambulio katika kipindi cha Pasaka.
                     Makundi ya Wakristo nchini humo yamesema 
yanadhani walipuaji walikuwa wakilenga kanisa moja lililo karibu na 
tukio, lakini kutokana na hali ya ulinzi iliyopo wakaamua kulipua nje 
kidogo.