May 31, 2011

IFUATAYO NI IDADI YA MAFISADI.....

JE UNAWAJUA MAFISADI WALIOTAJWA NA MH WILIBROARD SLAA? KAMA VIPI BOFYA HAPA,>>

May 29, 2011

SIO KUWA NAUZA SURA HAPANA WADAU...

Mambo  vipi  wadau  wangu  hapa  nipo  maeneo  magomeni.  nikiwa  karibu  kabisa  na  mdau  wangu  madishi... yaani  jamaa  hadi  home  kwangu  kaja  kunisetia    black and white  tv..  du  hata mpira  nilifaidi..  huyu  jamaa  noma.  wewe  kama  unataizo  lako  la  dish  mstustue  tu  huyu  jamaa..  au  mtembeleeni  katika  web  yake  ya  blog.  ni  mustaphamadish.blogspot.com  ujionee  mwenyewe..  hata  kama  tv  yako  ni  black and white  atakurekebishia  kwa  dish  mpaka  chanel  tuliiii!!!!!!!  kama  vip  wewe    soma  mwangajamii...

{KIMATAIFA}Mubarak atozwa faini dola milioni 90....

Mahakama ya Misri yameamrisha faini ya dola milioni 90, atozwe rais wa zamani, Hosni Mubarak, pamoja na maafisa wake wawili, kwa kukata huduma za simu za mkononi wakati wa maandamano dhidi ya serikali mwezi wa Januari.
Hosni Mubaraka na mkewe, Heidi, na watoto Gamal (kulia, na Alaa
Hiyo ndiyo hukumu ya mwanzo ya mahakama dhidi ya Bwana Mubarak.
Kiongozi huyo wa zamani anakabili mashtaka makubwa zaidi, kama kuamrisha waandamanaji kuuwawa, ambayo adhabu yake inaweza kuwa kifo.
Maafisa wawili waliotozwa faina na Bwana Mubarak ni waziri mkuu wa zamani, Ahmed Nazif, na waziri wake wa mambo ya ndani ya nchi, Habib al-Adly.



                                                                                                                                                             

 HUKO  LIBYA  TENA

NATO imeshambulia nyumba ya Gaddafi

NATO inasema kuwa imeangamiza minara ya walinzi katika eneo la nyumba ya Kanali Gaddafi wa Libya mjini Tripoli, kwa mashambulio mawili yaliyofanywa na ndege za umoja huo wa kijeshi.
Watu wakizungumza karibu na jumba la Gaddafi la Babu al_aziziya baada ya kushambuliwa mwezi Aprili
Waandishi wa habari mjini Tripoli, wanasema shambulio moja lilofanywa mchana, lilivunja sehemu za ukuta unaozunguka jengo la jeshi la Bab al-Aziziya.
Msemaji wa NATO, alieleza kuwa shambulio hilo ni funzo kubwa kwa kiongozi wa Libya, kwamba hawezi tena kujificha nyuma ya kuta ndefu.