April 07, 2012

HISTORIA FUPI YA MAREHEMU STEVEN KANUMBA

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgb139sjzqI0qacHRLNsK7lvE-fjPWEprK7-XrIeLK81VqysD18I2w0qcMvUQJ8cnQWQ-iOtxmvKwGale5wwt-0juEanVGeypNXjNV7Plykb1xOFmfK32YPhrPD5I2k6nPOARFUvR9JY83m/s1600/Steve+Kanumba.jpg 
HISTORIA YAKE:
Steven Charles Kanumbaa alizaliwa Januari 8, mwaka 1984 mkoani Shinyanga kabla ya umauti kumfiia Aprili 6, mwaka 2012.
Elimu ya msingi alipata katika shule ya Bugoyi, na baadaye akajiunga na  sekondari ya Mwadui, kabla ya kuhamia Dar Christian Seminary.
Baada ya kumaliza Kidato cha Nne Dar Christian, Kanumba alijiunga na sekondari ya Jitegemee, Dar es Salaam pia kwa elimu ya Kidato cha Tano na Sita.
Ni ni wakati huo akiwa Jitegemee Kanumba alianza shughuli za sanaa katika Kundi la Kaole Sanaa Group la Magomeni, Dar es Salaam.
Baada ya kukomaa Kaole, Kanumba aliamua kuanzisha kampuni yake mwenyewe ya filamu na hadi anakutwa na umauti alikuwa mwigizaji anayefahamika Afrika nzima.
Ameshirikiana na wasanii wakubwa duniani kama Ramsey Nouah wa Nigeria na amefanya kazi na mastaa wengine kadhaa wa Nigeria.
Miongoni mwa filamu ambazo alifanya ni Dar To Lagos, She is My Sister, Ancle JJ, Oprah, Tufani, Johari, Gharika, Baragumu, Sikitiko Langu, Dangerous Desire, Cross My Sin, Village Pastor, Family Tears na kadhalika.
Hivi karibuni, alikaririwa akisema atagombea Ubunge katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2015.
Kanumba atakumbukwa na wengi sana kwa ucheshi wake- upole na ushirikiano mzuri na wenzake katika kazi.
Kifo cha Kanumba ni pigo katika tasniya ya filamu Tanzania. Taifa limempoteza mtu ambaye alikwishaanza kuitangaza vema nchi kupitia sanaa hiyo na ambaye angetarajiwa kuitangaza zaidi katika anga za kimataifa zaidi kupitia sanaa hii.
Nigeria sasa wanajua Tanzania sasa filamu. Nchi nyingi za Afrika zinajua sasa nah ii sehemu ya kazi nzuri kwa Kanumba.
Mwenyewe aliwahi kukaririwa alifika hadi Hollywood hadi Marekani, ambayo ni ‘makka’ ya wacheza filamu. Kwa sasa mwili wa marehemu upo katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar es Salaam.
Mungu aiweke pema peponi roho ya marehemu. Amin.

MANENO YA STEVEN KANUMBA ENZI YA UHAI WAKE NA MOJA YA FILAMU ZAKE


steven kanumba  enzi  za  uhai  wake. hakika  maneno  na  kauli  zake  ni  kama  alitabiri

BREAK NEWSS STEVEN KANUMBA AMEFARIKI DUNIA.

STEVEN  KANUMBA  AFARIKI  DUNIA
Steven  kanumba  enzi  za  uhai  wake.  mungu  ailaze  roho  yake  mahali  pema  peponi  amen.

April 06, 2012

NAWATAKIA WAKRISTO WOTE IJUMAA KUU NJEMA.


April 05, 2012

KWA MFUMO HUU WATANZANIA TUTAFIKA?

Kutokana na uchunguzi uliofanyika na mwangajamii imegundulika kuwa makampuni mengi ya ujenzi tanzania yanatabia ya kunyonya wafanyakazi ili neno kunyonya ni neno la kawaida tu. kwa mfano samaki anayeitwa sangara ambaye ni samaki anaekula samaki wenzake nikiwa na maana ni wale samaki wadogo. hivi majuzi mwangajamii iliweza kutia mguu katika maeneo ya pale upanga jijini dar es salaam kwa kampuni moja inayoitwa mohamed belder limited ambapo bila kujali lolote nilijichanganya na mimi kuomba kibarua cha kubeba zege nia na madhumini nikujua wafanyakazi wanalipwa vipi na ni shilingi ngapi. hatimae niligundua kuwa kiwango cha fedha ni kidogo sana wanaolipwa vibarua wa kawaida kwani hulipwa shilingi 5000 hadi 6000. na nikiwango kidogo sana kwa maisha ya sasa hivi. nahaidi kuweka picha na baadhi ya wafanyakazi katika blog hii hivi karibuni. wadau kaeni mkao wa kula.

NAWATAKIA WAKRISTO BASAKA NJEMA NA KILA LA KHERI:

Mbuzi  wa  pasaka

April 04, 2012



Maafisa wa michezo wauawa Somalia



Wajumbe wa Kamati ya Olimpiki ya Somalia na viongozi wa chama cha kandanda cha Somalia ni miongoni   mwa watu saba waliouwawa katika shambulio la bomu mjini Mogadishu.



jumba la tamthilia Somalia    
Wanaharakati wa kundi la al-Shabab wanasema ndio waliotekeleza shambulio hilo.
Jeshi la kuweka amani la Muungano wa Afrika nchini Somalia limelaani shambulio hilo kua ni kitendo "kinachokirihisha" na kusema hakitavuruga juhudi za amani.
Rais wa Kamati ya Olimpiki ya Somalia , Aden Yabarow Wiish, na mkuu wa shirikisho la kandanda nchini Somalia , Said Mohamed Nur, nao pia waliuwawa. Walikua ni miongoni mwa kikundi cha wageni mashuhuri waliokusanyika kuadhimisha mwaka mmoja tangu kuanzishwa kwa kituo cha televisheni ya taifa ya Somalia.
Rais wa shirikisho la kandanda la kimataifa FIFA ,Sepp Blatter, alisema ameshtushwa sana kwa vifo vya maafisa hao wa michezo.
Waandishi habari watatu wa kituo cha televisheni cha Somalia nao pia walijeruhiwa kwa mujibu wa rubaa zilizoiarifu idhaa ya Kisomali ya BBC.
Jumba hilo la tamthilia lilifungwa katika miaka ya mwanzo ya 1990 wakati Somalia ilipotumbukia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe na lilifunguliwa upya mwezi mmoja tu uliopita wakati wa awamu mpya ya matumaini ya kurejea amani.
Waziri mkuu Abdiweli alisema mwanamke aliyejitoa mhanga ndie aliyefanya shambulio hilo.
Akilaani kundi la al-Shabab, alisema ni kawaida yao "kuwaua watu wasio na hatia ".
Salah Jimale,aliyeshuhudia shambulio hilo ameliambia shirika la habari la Associated Press " Mlipuko huo ulitokea wakati wapiga muziki walikua wakiimba huku wakishangiliwa na watazamaji.
"Moshi mweusi ulitanda kila mahali. Watu walipiga mayowe na wanajeshi ghafla wakaanza kufyatua risasi katika lango la kuingia ndani."
Waandishi wa habari waliokuwepo hapo wanasema watu kadhaa walijeruhiwa na wanaelezea kuona viatu na simu za mkononi vilivyojaa damu,na viti kulipuliwa vipande vipande na mlipuko huo.
Katika taarifa yake kundi la al-Shabab limesema ndilo liliohusika na shambulio hilo lakini limezungumzia bomu lililotegwa badala ya mshambuliaji wa kujitoa mhanga.
Msemaji wa Al-Shabab Sheikh Abdiasis Abu Musab ameliambia shirika la habari la Reuters "sisi ndio tuliopanga mlipuko katika jumba la tamthilia. Tuliwalenga mawaziri na wabunge makafiri na ndio miongoni mwa maafa ya leo."
Wanaharakati hao walitimliwa kutoka Mogadishu na wanajeshi wa Muungano wa Afrika mnamo mwaka jana.
Tangu wakati huo kumekuwepo na kipindi cha utulivu kiasi ambapo shughuli za michezo zilianza upya,mikahawa kufunguliwa pamoja na jumla la taifa la tamthilia.
Lakini al-Shabab imeendelea kushambulia mji mkuu kwa mabomu na makombora. .
Wakati huo huo,mjumbe maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika mzozo wa Somalia, Augustine Mahiga ameelezea kukerwa kwake na shambulio hilo katika Jumba la Tamthilia la Kitaifa

BREAKNEWSSS!! SOKO LA FERI JIJINI DAR ES SALAAM LANUSURIKA KUTEKETEA NA MOTO.


SOKO  LA  FERI  JIJINI  DAR ES SALAAM