June 15, 2012

(FIKRA MBADALA) NINI KIFANYIKE KUONDOKANA NA MAAFA KAMA HAYA?

Katika  kipindi  kilichopita ndugu  zetu  walipoteza  maisha  kwa  mafuriko  na  hii  yote  ni  kutokana  na  kukosa  maarifa. na  walioathirika  zaidi  na  mafuriko  yale  asilimia  kubwa   ni  wapangaji.  ila  wenye  nyumba  ni  asilimia  ndogo  sana.  kwa  hiyo  napenda  kusema  kuwaondoa  wananchi  katika  maeneo  ya  bondeni  kiukweli  inakua  ngumu  sana   kutokana  kwamba  kunabaadhi  ya  watu  wanakaa  bondeni kwa  kukimbia  gharama  za  kode  za  vyumba.  mfano  mmoja  hivi  majuzi  mwangajamii  imefanya  uchunguzi  na  kugundua  vyumba  vingi  vya  bondeni  bei  zake  ni  ndogo  ukilinganisha  na  visivyo  vya  bondeni  gharama  zake  ni   kubwa.  na  ndio  maana  wananchi  wenye  kipato  cha  chini ndio wanakimbilia  mambondeni. na  endapo  mvua  zikanyesha  wanakuwa  matatizoni.  nataka  kuipatia serikali  ushauri.  kama  kuna uwezekano    maeneo  ya mabondeni serikali  Ichimbe mitaro mikubwa  ambayo  itaelekeza  maji   kwenda baharini pale  mvua  zitakaponyesha.... Tusikubali  watanzania  wafe  kwa  kukosa maarifa  na  ikiwezekana  hata  michango  ipita  kwa  wale  wote  wanaishi  mambondeni  ili  kukamilisha programu  hiyo..

June 11, 2012

(KIMATAIFA) HUKO LIBYA TENA.. ICC IMEFANYA NINI ENDELEA KUSOMA.


Ajami al-Ateri kiongozi wa kundi la wapiganaji la Zintan brigade, linalomzuilia Saif al-Islam Gaddafi

Maafisa wanne wa mahakama ya ICC nchini Libya wamewekwa jela. Taarifa hizi ni kwa mujibu wa kundi moja la wapiganaji nchini Libya.
Inaarifiwa wanne hao walizuiliwa mnamo Alhamisi na wataendelea kufungwa kwa siku 45 wakisubiri uchunguzi.
Mmoja wa maafisa hao , wakili Melinda Taylor, anatuhumiwa kwa kujaribu kumkabidhi stakabadhi mwanawe hayati Muamar Gaddafi, Saif al-Islam Gaddafi anayezuiliwa na kundi la wapiganaji la Zintan brigade ambalo limekuwa likimzuilia tangu mwezi Novemba.
Wanne hao walihamishwa hadi jela kwa amri ya mwanasheria mkuu na maafisa wa wizara ya ulinzi, kulingana na Ajami al-Ateri kiongozi wa kundi hilo la Zintan brigade.
Ateri alifahamisha BBC kuwa maandamano yatafanyika kutaka wanne hao kufunguliwa mashtaka.
Taarifa za wizara ya mambo ya nje ya Libya zilithibitisha wanne hao kuzuiliwa kwa siku 45 ingawa alikanusha kuwa wako jela.
Maafisa wa utawala nchini Australia wamesema wanatafuta njia za kidiplomasia kuweza kumfikia mmoja wa wajumbe hao Bi Taylor ambaye ni raia wa nchi hiyo pamoja na maelezo kuhusu sababu zililosababisha kuzuiliwa kwake.
Ujumbe mwingine wa ICC uliwasili nchini Libya mnamo Jumapili, katika juhudi za kutaka maafisa hao kuachiliwa.
 Saif al Islam

Hii leo maafisa wa serikali ya Libya wamesema wanashauriana kuweza kukutana na wajumbe hao eneo la Zintan hapo kesho.
Wanachama wa kundi hilo la Zintan wanadai kuwa wajumbe hao walikuwa wamebeba nyaraka ikiwemo barua kutoka kwa rafiki wa karibu wa Saif A Islam ambaye yuko nchini Misri.
Inaarifiwa barua hiyo ilikuwa na picha pamoja na alama ambazo zilieleweka tu kwa mwenye kuutuma ujumbe huo pamoja na Saif al-Islam mwenyewe, alisema balozi wa Libya katika mahakama ya ICC.
Saif al-Islam, alikamatwa Novemba mwaka jana na kundi hilo la wapiganaji wakati akijaribu kutoroka. Anatakikana na ICC kwa tuhuma za ukiukwaji wa haki za binadamu.
Ingawa serikali ya muda ya Libya imekataa kumkabidhi kwa ICC iksema ni bora mahakama ya Libya iweze kusikiliza kesi dhidi yake.