Katika kipindi kilichopita ndugu zetu walipoteza maisha kwa mafuriko na hii yote ni kutokana na kukosa maarifa. na walioathirika zaidi na mafuriko yale asilimia kubwa ni wapangaji. ila wenye nyumba ni asilimia ndogo sana. kwa hiyo napenda kusema kuwaondoa wananchi katika maeneo ya bondeni kiukweli inakua ngumu sana kutokana kwamba kunabaadhi ya watu wanakaa bondeni kwa kukimbia gharama za kode za vyumba. mfano mmoja hivi majuzi mwangajamii imefanya uchunguzi na kugundua vyumba vingi vya bondeni bei zake ni ndogo ukilinganisha na visivyo vya bondeni gharama zake ni kubwa. na ndio maana wananchi wenye kipato cha chini ndio wanakimbilia mambondeni. na endapo mvua zikanyesha wanakuwa matatizoni. nataka kuipatia serikali ushauri. kama kuna uwezekano maeneo ya mabondeni serikali Ichimbe mitaro mikubwa ambayo itaelekeza maji kwenda baharini pale mvua zitakaponyesha.... Tusikubali watanzania wafe kwa kukosa maarifa na ikiwezekana hata michango ipita kwa wale wote wanaishi mambondeni ili kukamilisha programu hiyo..
0 Comments