Maelfu ya watu wamejitokeza
kutazama mwenge wa Olimpiki ukipita, kuanza safari ya kutembezwa kwa
siku 7 sehemu mbali-mbali za Uingereza, kabla ya michezo ya London mwezi
wa Julai.
Mwenge huo utatembezwa na watoto, watu waliojitolea, pamoja na wanariadha, kabla ya kufikishwa kwenye uwanja wa Olimpiki mjini London, tarehe 27 Julai.
0 Comments