IKUMBUKWE SIKU YA AJALI HIZI!!

http://api.ning.com/files/i5a-gAU4NOfGEv70zRzWXCiTJUmaSeDFjMUjE-LU0oO1E1J5EQ5xOKdlXxykEjgx8LNhwY5FcOwkn2HqEL2R8yv3jqPHY*-2/MELII.jpg

 NI  MIONGONI  MWA  AJALI  AMBAZO  ZILISABABISHWA  NA  UZEMBE  WA  SUMATRA  AMBAYO  NDIO  WENYE  MAJUKUMU  YA  KUANGALIA  USALAMA  WA  VYOMBO  VYA  USAFIRISHAJI.

NAWEZA  KUSEMA  KUWA  KWA  MFUMO  HUU  WA  KUANGALIA  MATUMBO  YENU  NA  KULIPWA  FEDHA  ZISIZOKUWA  NA  TIJA  NA  WANANCHI  ZITAWATOKEA  PUANI.  SUMATRA  HAWAKO  MAKINI  KWA  USALAMA  WA  VYOMBO  VYA  NCHI  KAVU  NA  MAJINI.  KWA  SABABU  WANAJUA  HATA  WASIPOSHUGHULIKIA  SWALA  MUHIMU  KAMA  HIZO  PESA  ZITAINGIA  TU.  KWA  NAMNA  MOJA  AU  NYINGINE  RUSHWA  INACHANGIA.  UTASHANGAA  RUSHWA  INATEMBEA  MPAKA  KWENYE  ROHO  ZA  WATU.  KWA  MFANO  MELI  INATAKIWA  KUBEBA  WATU  400 CHA  KUSHANGAZA  UTAONA  MELI  IMEBEBA  WATU 800.  EBU  JIULIZE  KAMA  SI  RUSHWA  IMETEMBEA,  JE  HIYO  MELI  INGEBEBA  HAO  WATU? JIBU  NI  HAPANA.  NA  MWANANCHI  NI  KAMA  KONDOO  ANAKUSILIZA  WEWE  KIONGOZI  WEWE   NDIO  MSINGI  WAKE.  USIFIKIRI  UKIANDIKA  BANGO  UKAWEKA  NJIANI  KWAMBA  WATU  WOTE  WATAWEZA  KUSOMA,,    HAPA  SIKWELI  WEKA  BANGO  PAMOJA  NA  VITENDO  VIWEPO.  TUMEPOTEZA  NDUGU  ZETU  KWA  UZEMBE  WA   SERIKALI   KUWEKA  CHOMBO KIBOVU(SUMATRA) PAMOJA  NA  UKOSEFU  WA  VIWANGO.(TBS)

 

 

AJALI  YA  TRENI  MWAKA 2009:

 


 

Unakumbuka: MIAKA 13 AJALI YA MV BUKOBA

Mv Bukoba baada ya kugeuka chini juu.Hiyo sehemu yenye rangi nyeusi ni sehemu ambayo kawaida inakuwa chini ya maji .Walikuja watu(bila kujua wanafanya nini) walikata sehemu hiyo mbele chini yenye "ombwe" na kufanya kama pulizo lililotobolewa na meli ikazidi kuzama
Hili ni bango lilipo kwenye makaburi ya pamoja yaliyopo Igoma jiji Mwanza.Kutokana na miili ya walio wengi kuharibika na maji na hivyo kushindwa kutambuliwa na sababu zingine ilipelekea wapendwa wetu wapumzishwe kwenye makazi yao ya kudumu hapo.
Mnara wa kumbukumbu ya ajali ya Mv Bukoba,wenye orodha yabaadhi ya majina ya waanga wa ajali.Nilisimama eneo hilo siku ya tukio na kuweza kuona kwa mbali eneo ambalo ajali ilikuwa imetokea tukiwa na watu wengine.Mnara umejengwa kwenye shule ya wasicha Bwiru.

Mei 21,1996 katika ziwa Victoria,Mwanza Tanzania meli ya Mv Bukoba ilipata ajali na zaidi ya watu 800 kupoteza maisha yao.Meli ilizama kilomita 30 kukaribia kutua nanga kwenye bandari ya mwanza ikitokea Bukoba.
Meli ikuwa na uwezo wa kubeba idadi ya watu 430. Kwenye first and second class orodha ya abiria ilikuwa 443 na kwenye third class hakukuwepo rekodi yoyote .Takribani 1000 walifariki kwenye ajali hiyo.

Afrika ya kusini ilibidi kutoa msaada wa wanamaji wake waje kutusaidia kufanya uzamiaji wa kina kirefu kwani tulikuwa hatuna hivyo vifaa na utalaamu(sijui inagharimu kiasi gani kuvipata vifaa na utalaamu)

Meli ilikuwa na ubovu lakini iliruhusiwa kuendelea na kazi kama kawaida.(nani anajali au kuwajibishwa?)

Vifaa vya uokoaji mfano majaketi(life jacket) n.k na vitu kama hivyo vilikuwepo vya kutosha?( au hakuna uzembe wa viongozi..ni kazi ya Mungu kama walivyozoea kusema)


SWALI LA MSINGI!!!!!
hivi Serikali imeshindwa kutenga japo dakika 3 nchi nzima kusimama kuwakumbuka ndugu zetu waliotutoka kutokana na uzembe wa watendaji wa serikali?

Kama wanaweza kukusanya mamilioni kusherekea sherehe za kisiasa inagharimu nini kutoa tamko kuhusu hiyo siku.

Poleni sana wafiwa..tupo pamoja ..mwenyezi Mungu awapumzishe mahala pema peponi woote waliotangulia mbele ya haki.Amina

Post a Comment

1 Comments

Anonymous said…
Lilikuwa ni pigo kubwa sana tanzania. hakika ni historia ambayo haitasahaulika daima....by Ramadhani from majengo moshi...