RAIS JAKAYA KIKWETE AKIMKABIDHI ZAWADI YA KINYAGO WAZIRI MKUU WA INDIA.
Rais Jakaya Kikwete akimkabidhi zawadi ya kinyago Waziri Mkuu wa India, Dk Manmohan Singh wakati Waziri Mkuu huyo alipokutana naye Ikulu, Dar es Salaam. Waziri Mkuu huyo anatarajiwa kurejea nchini kwake Mei 28
MALUMBANO YA JANA YALIYOKUWA YAKIRUSHWA NA ITV KUHUSU NINI KIFANYIKE NINI ILI KUZUIA AJALI, NI ABIRIA MWENYE AWE ANASHIRIKIANA NA JESHI LA POLISI KATIKA KUONDOA ONGEZEKO LA AJALI BARABARANI... NI MCHANGO WANGU TU HUO..
[KIMATAIFA]>>>>>Na huko sudan wenye silaha Sudan 'wachoma moto Abyei...
^Wakimbizi wakiukimbia mji wa Abyei^
Majeshi ya kutunza amani ya Umoja wa Mataifa nchini Sudan yamesema mji unaozozaniwa uliopo mpakani Abyei umechomwa moto tangu ulipotekwa na majeshi kutoka kaskazini. Umesema majeshi ya Sudan, yanayoitii serikali ya kaskazini, yalikuwa na jukumu la kuhakikisha sheria inafuatwa Abyei. Takriban wakazi 20,000 wameukimbia mji huo katika siku za hivi karibuni. Abyei umekuwa na hali ya wasiwasi mkubwa tangu upande wa kusini kupiga kura mapema mwaka huu kutaka kujitenga na upande wa kaskazini. Baraza la usalama la umoja wa mataifa linatarajiwa kujadili mtafaruku huo na Rais wa Sudan kusini.