March 29, 2012

HABARI ZA KIMATAIFA:


Ikulu ya rais nchini Mali
Kumekuwa na shutma za kimataifa dhidi ya wanajeshi wa Mali waliopindua serikali ya rais Amadou Toumani Toure. 
 
Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limetaka utawala wa kikatiba kurejeshwa nchini humo, huku Benki ya Dunia pamoja na Benki ya Maendeleo barani Afrika wakisema wanasitisha baadhi ya shughuli nchini humo.
Msemaji wa wanajeshi waasi nchini Mali amesema jeshi litarejesha demokrasia nchini humo na kuwa umoja utarejea hivi karibuni.
Kufikia sasa haijulikani alipo Rais Amadou Toumani Toure, lakini taarifa ya televisheni ya taifa ilisema kuwa rais huyo yuko katika hali nzuri ya kiafya.
 

TULIMPENDA SANA LAKINI MUNGU ALIMPENDA ZAIDI.

Ni  mwandishi  wa  habari  wa  itv  na  radio one stereo  ambaye  alitutoka  majuzi.  hapo  ndipo  makao makuu  yake  ya  milele,  mungu  aiweke  roho  yake  pahali  pema  peponi (Amen)

March 27, 2012

TUNADUMISHA MILA.

 





Mtoto wa jamii ya wafugaji wa kabila la Kimasai mkazi wa kitongoji cha Makuture, Dakawa wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro ambaye jina lake halikufahamika akinyonya maziwa ya ng’ombe kwa kutumia kibuyu huku akiwa amelala miguuni mwa mama yake.

HAWA VIONGOZI WA SERIKALI YA TANZANIA WANATUTAKIA NINI SISI WATANZANIA?

Swala  la  umeme  tanzania  limekuwa  kero.  kwani  mamilioni  ya watanzania  wanategemea  nishati  ya  umeme  kuendesha  mambo  yao  ikiwemo  kuhifadhi  bidhaa  mbalimbali.  lakini  leo   hii  serikali  inasubutu  kutikisa  kiberiti  kwa  kuwaambia  wananchi .   @ nchi  ipo  karibuni  kuingia   gizani.  nikisema  hivyo  kama  mwandishi  wa  habari  hii.    inafikia  hatua  napeleka  mawazo  yangu  nakusema  ni  bora  hata  hao  waigereza    warudi  tu  kuitawala  tanzania  tena  kwa  mara  ya pili. nahisi  watanzania  wengi  sasa  hivi  wamefilisika  kutokana  na  hali  ngumu  ya  maisha.  hii  nikutokana  na  mifumo  mibovu  ya  viongozi  wa serikali.  @  kuna msemo wanakuambia    wewe  mwananchi  ndio  serikali  hii  ni  sawa  na danganya  toto  ya  kumpa  pipi  Asilie, maneno  hayo  yananichoma  sana  sana.  wanatufunga  macho  na  biskuti  na  wakati  tunaweza  kuivunja.  sasa  wakati  umefika  kwa  watanzania kutaka  kieleweke.  nafahamu  kuwa  mnatupiga  vita  sana  waandishi  wa  habari  kwa  kuwa   tunawahabarisha wananchi  maovu  yenu.  Sasa  leo  hii  tunaona  shirika  la  tanesco  limegeuzwa  kama  godoro  kodi  walipe  wao  bado  mnataka  waendelee kutoa  huduma.  bado  Tanesco  inawadai  nyie  vigogo  pamoja  serikali  lakini  mnajifanya  hamuoni  wala  hamsikii. Kwa  taarifa  yenu  sasa  hivi  kila  mwananchi  anajua  kuwa  hiyo  tanesco haihusiki  na  umeme  ila  wahusika  ni  nyie.  Viongozi  wasirikali  huu  mwaka   si  wa  mabwege  tena  kwa  watanzania  wengi  wamesoma   na  si  enzi  la  mwalimu  nyerere

March 25, 2012

KARNE YA MABAUNSA.

   Kwa  mfumo  huu  ndani  ya  mwaka    2020  patakuwa  shika  nguo  kuchanika: