January 23, 2012

MAZINGIRA YANAANZA NA WEWE....

KWA  MAZINGIRA  MENGINE  INATUBIDI  TUSIILAUMU  SERIKALI. HIVI  MAJUZI   NILIKATIZA  MAENEO  YA  SOMANGA  PALE MAKABURINI  KIUKWELI  MAZINGIRA  NI  MACHAFU  SANA.  HII  INATOKANA  NA  WANANCHI  WENYEWE  KUSHINDWA  KUJIELEWA  KUWA MUDA   WOWOTE  KUNAWEZA  KUIBUKA   MAGONJWA  YA TUMBO. KAMA KIPINDUAPINDUA. INANISIKITISHA SANA  ENDAPO  NITASIKIA  MWANANCHI  ANALALAMIKA  KUWA. SERIKALI  HAIMTENDEI  HAKI    BILA  KUFAHAMU  KUWA  YEYE  MWENYEWE  NDIO  CHANZO  CHA  MATATIZO.  KWA  NAMNA  HII  JIJI   HILI  LA DAR ES SALAAM  UCHAFU  HAUTOWEZA  KUTOKOMEA.  MTANZANIA  HII  NA  WEZA  KUSEMA   NI  KUTOKUWA  NA MPANGILIO  WA  MAISHA  YA  KILA  SIKU.. NA  UTUMWA  SI  MPAKA.  KUTUMISHA  NA  BINADAMU  MWENZIO    HATA  MAZINGIRA  YANAWEZA  KUKUFANYA  UKAWA  MTUMWA. LABDA  UJANIELEWA.  INAMAANA  UKIPATWA NA  MAGONJWA BASI  WEWE NI  MTUMWA   WA MAGONJWA.

January 22, 2012

Ghasia zaendelea Nigeria

 Watu kama wanane inaarifiwa kuwa wamekufa katika mashambulio mengine kaskazini mwa Nigeria.


Katika mji wa Tafawa Balewa kwenye jimbo la Bauchi, kituo cha polisi kilishambuliwa na mapambano ya risasi yalitokea baina ya polisi na watu waliokuwa na bunduki.
Inaarifiwa kuwa mwanajeshi mmoja aliuwawa kwenye kituo cha ukaguzi katika eneo jengine.
Makamo wa rais wa Nigeria, Namadi Sambo, yuko njiani kuelekea mji wa Kano, ambako watu kama 100 waliuwawa kwenye miripuko kadha ya mabomu Ijumaa usiku.
Chama cha wapiganaji wa Kiislamu cha Boko Haram kilidai kuhusika na mashambulio ya mjini Kano.