NI MIONGONI MWA AJALI AMBAZO ZILISABABISHWA NA UZEMBE WA SUMATRA AMBAYO NDIO WENYE MAJUKUMU YA KUANGALIA USALAMA WA VYOMBO VYA USAFIRISHAJI.
NAWEZA KUSEMA KUWA KWA MFUMO HUU WA KUANGALIA MATUMBO YENU NA KULIPWA FEDHA ZISIZOKUWA NA TIJA NA WANANCHI ZITAWATOKEA PUANI. SUMATRA HAWAKO MAKINI KWA USALAMA WA VYOMBO VYA NCHI KAVU NA MAJINI. KWA SABABU WANAJUA HATA WASIPOSHUGHULIKIA SWALA MUHIMU KAMA HIZO PESA ZITAINGIA TU. KWA NAMNA MOJA AU NYINGINE RUSHWA INACHANGIA. UTASHANGAA RUSHWA INATEMBEA MPAKA KWENYE ROHO ZA WATU. KWA MFANO MELI INATAKIWA KUBEBA WATU 400 CHA KUSHANGAZA UTAONA MELI IMEBEBA WATU 800. EBU JIULIZE KAMA SI RUSHWA IMETEMBEA, JE HIYO MELI INGEBEBA HAO WATU? JIBU NI HAPANA. NA MWANANCHI NI KAMA KONDOO ANAKUSILIZA WEWE KIONGOZI WEWE NDIO MSINGI WAKE. USIFIKIRI UKIANDIKA BANGO UKAWEKA NJIANI KWAMBA WATU WOTE WATAWEZA KUSOMA,, HAPA SIKWELI WEKA BANGO PAMOJA NA VITENDO VIWEPO. TUMEPOTEZA NDUGU ZETU KWA UZEMBE WA SERIKALI KUWEKA CHOMBO KIBOVU(SUMATRA) PAMOJA NA UKOSEFU WA VIWANGO.(TBS)
AJALI YA TRENI MWAKA 2009:
Unakumbuka: MIAKA 13 AJALI YA MV BUKOBA
Mv
Bukoba baada ya kugeuka chini juu.Hiyo sehemu yenye rangi nyeusi ni
sehemu ambayo kawaida inakuwa chini ya maji .Walikuja watu(bila kujua
wanafanya nini) walikata sehemu hiyo mbele chini yenye "ombwe" na
kufanya kama pulizo lililotobolewa na meli ikazidi kuzama
Hili
ni bango lilipo kwenye makaburi ya pamoja yaliyopo Igoma jiji
Mwanza.Kutokana na miili ya walio wengi kuharibika na maji na hivyo
kushindwa kutambuliwa na sababu zingine ilipelekea wapendwa wetu
wapumzishwe kwenye makazi yao ya kudumu hapo.
Mnara
wa kumbukumbu ya ajali ya Mv Bukoba,wenye orodha yabaadhi ya majina ya
waanga wa ajali.Nilisimama eneo hilo siku ya tukio na kuweza kuona kwa
mbali eneo ambalo ajali ilikuwa imetokea tukiwa na watu wengine.Mnara
umejengwa kwenye shule ya wasicha Bwiru.
Mei 21,1996
katika ziwa Victoria,Mwanza Tanzania meli ya Mv Bukoba ilipata ajali na
zaidi ya watu 800 kupoteza maisha yao.Meli ilizama kilomita 30
kukaribia kutua nanga kwenye bandari ya mwanza ikitokea Bukoba.
Meli ikuwa na uwezo wa kubeba idadi ya watu 430. Kwenye first and second class orodha ya abiria ilikuwa 443 na kwenye third class hakukuwepo rekodi yoyote .Takribani 1000 walifariki kwenye ajali hiyo.
Afrika
ya kusini ilibidi kutoa msaada wa wanamaji wake waje kutusaidia kufanya
uzamiaji wa kina kirefu kwani tulikuwa hatuna hivyo vifaa na utalaamu(sijui inagharimu kiasi gani kuvipata vifaa na utalaamu)
Meli ilikuwa na ubovu lakini iliruhusiwa kuendelea na kazi kama kawaida.(nani anajali au kuwajibishwa?)
Vifaa vya uokoaji mfano majaketi(life jacket) n.k na vitu kama hivyo vilikuwepo vya kutosha?( au hakuna uzembe wa viongozi..ni kazi ya Mungu kama walivyozoea kusema)
SWALI LA MSINGI!!!!!
hivi
Serikali imeshindwa kutenga japo dakika 3 nchi nzima kusimama
kuwakumbuka ndugu zetu waliotutoka kutokana na uzembe wa watendaji wa
serikali?
Kama wanaweza kukusanya mamilioni kusherekea sherehe za kisiasa inagharimu nini kutoa tamko kuhusu hiyo siku.
Poleni sana wafiwa..tupo pamoja ..mwenyezi Mungu awapumzishe mahala pema peponi woote waliotangulia mbele ya haki.Amina
1 Comments