KWANINI WAKULIMA WENGI SANA NCHINI TANZANIA WAMEKUWA NA HALI NGUMU . KWA WANAPOCHUKUA MIKOPO, NA HATIMAYE KUSHINDWA KURUDISHA MIKOPO HIYO SEHEMU HUSIKA?

{MAENDELEO  KWANZA  NA  SI  KILIMO  KWANZA}








LEO  NIMEAMUA   KWENDA  KWENYE  MASWALA  YA  KILIMO...  NIKIWA  NA  NIA  NA  MPANGO  PAMOJA  NA  USHAURI  NDANI  YA  SERIKALI  YANGU YA TANZANIA. KUHUSU KILIMO.!!

Niliweza  kutembelea  kata  moja   hivi  iliyopo  mkoa  wa  kilimanjaro  wilaya  ya  mwanga    kwa  jina  Jipendea..  kata  hii  ipo  katika  wilaya  ya  mwanga.. kwani  nilishangazwa  na  kuona  maeneo  makubwa  sana  ya  kilimo...  kwani  nilimuuliza  mwenyeji  wangu  kwanini  watu  wa  kata  hii  ya  jipendea  wanalalamikia   swala  la  kukosa chakula  na  wakati  wanamashamba?  mwenyeji  yule  alinijibu    " mmm  ndio  maeneo  kibao  ya  kulima  lakini  ukame  umezidi"  nikamwambia  kwanini?  hakujibu    na nikauliza nilishawahi   kuambiwa  maeneo  ya  kata  ya  jipendea  maji  yanapatikana  kiurahisi..?  Kaniju"hapana  kipindi  hiki  ni  cha  kiangazi  na  ndio  sababu  watu  hawawezi  kulima  na  maji  yaliyopo nimadogo."  kwani.  niliendelea  kumuuliza  maswali  ya  kuhusu upatikanaji  wa  agricuture. aliniambia  watu  hao  wapo  lakini  wapo  tu  kama  bosheni lakini  hatujawahi  kuona  ametembelea  shamba  lolote  na  kutoa  elimu  juu  ya  kilimo.

Kulingana  maelezo  niliyoyapata  kutoka  kwa  mwenyeji  wangu  huyo  nilijua  moja kwa  moja  wanakijiji  wa  kata  ya  jipendea  hawana  elimu  ya  kilimo.. na  nikagundu    kumbe  ndio  maana  unakuta  watu  wanakopa  fedha  kutoka  mashirika  ya  kukopesha mf:sacos  mwisho  wanashindwa  kurejesha   mkopo  waliyokopa  yote  hayo  ni  kutokana  na kukosa  elimu  ya  kilimo.
Sasa  kama  mkulima  anakopa  kisha  anashindwa  kulipa  mkopo  huo  je  kunauwezakano  wa  kuwepo  kwa  maendeleo?  jibu  ni  hapana.  ila  mimi  napendekeza  elimu  lazima  itolewe   kwa  wakulima,  kumbuka  kuwa  mkulima  ndio  kiungo  kikubwa  tanzania  na  hata  duniani.  lakini  leo  hii  mkulima  anaechipukia  kwa  kilimo  kisha  mkamnyima  elimu  ya  kilimo  manategemea  nini.?kazi  kweni  serikali..

katika  sehemu  nyinge  naona  ni  bora    hayo  mashirika  ya  kukopesha  kwanini  yasitoe  ushauri  kwa wakulima  wanaokopesha..  ikiwemo  kushirikiana  na   ma bwana shamba  kuwapa elimu  na  pia  ushauri  na  kuwapa  mfumo  mzima  wa  kilimo  cha  kisasa..?  lakini   kinachoniuma  mimi  kama  mwangajamii  nipale  mkulima  mpaka  leo  anatumia  jembe  la  mkono.. na  sio.  kuwa  anapenda  ni  kwa sababu  ya  vifaa  vya kisasa  kuwa  na  gharama  kubwa.  na  ukilinganisha na kipato  cha  mtu  anaishie  vijijini  ni  kidogo..   kiukweli  labda  mtu  ana mlo mmoja  kwa  siku  alafu  umwambie  maswala  ya  power tiler hawezi  kukuelewa...  hata  akikopeshwa  bado  riba  yake  nikubwa  na  uwezi  kumpa  power tiler  kama  elimu  hana  ya  kilimo..  cha  muhimu  ni  serikali  ya  tanzania  kuweka  mkakati  wa  kupeleka  ma  bwana shamba  wa  kutosha  na  hao  ma bwana shamba wawajibike  na  sio  kula  bata  tu.  leo  hii  mnatuambia  oohh    kilimo  kwanza  nahisi  kama  ni  jocking  kwa  wananchi  wa  vijijini.    na  ukitazama  Tanzania  imebarikiwa   maeneo  makubwa.  na  inauwezo  wa  kusambaza  chakula  afrika  nzima  lakini  uongozi    hauko  makini  na  rasilimali  ya  tanzania.  ila  wanafaidika  watu  wa  nje.  huku  watanzania  tukipiga  mihayo  ya  njaa    wengine  wakila  na  kusaza..  Eti  tanzania  nchi  yangu  ingekuwa  nchi  yako    usingekufa  na njaa...

narudia  tena    KILIMO  KWANZA  0%    ila  serika  naomba  ikaze  buti  kimaendeleo  hususani  ya  kilimo...   

Post a Comment

6 Comments

Anonymous said…
kwani hilo geni kwa watanzania?
Anonymous said…
viongozi wetu wako kimaslahi peke yake na si kimaendeleo..
Anonymous said…
wezi mtupu...
Anonymous said…
Kuna wataalamu wanafika ila ni wachache sana ni srikali ingejaribu kidogo.. kuongeza wataalam vijijini..
Anonymous said…
wenye uwezi ndio pekee wanawekununua vifaa vya kisasa vya kilimo kwa 7babu gharama yake kubwa.. na ndio maana walala hoi hamudu.
Anonymous said…
mali tunazo lakini tunashindwa kutumia kwasababu tu hatuna utaalamu.