{MAENDELEO KWANZA NA SI KILIMO KWANZA} |
Niliweza kutembelea kata moja hivi iliyopo mkoa wa kilimanjaro wilaya ya mwanga kwa jina Jipendea.. kata hii ipo katika wilaya ya mwanga.. kwani nilishangazwa na kuona maeneo makubwa sana ya kilimo... kwani nilimuuliza mwenyeji wangu kwanini watu wa kata hii ya jipendea wanalalamikia swala la kukosa chakula na wakati wanamashamba? mwenyeji yule alinijibu " mmm ndio maeneo kibao ya kulima lakini ukame umezidi" nikamwambia kwanini? hakujibu na nikauliza nilishawahi kuambiwa maeneo ya kata ya jipendea maji yanapatikana kiurahisi..? Kaniju"hapana kipindi hiki ni cha kiangazi na ndio sababu watu hawawezi kulima na maji yaliyopo nimadogo." kwani. niliendelea kumuuliza maswali ya kuhusu upatikanaji wa agricuture. aliniambia watu hao wapo lakini wapo tu kama bosheni lakini hatujawahi kuona ametembelea shamba lolote na kutoa elimu juu ya kilimo.
Kulingana maelezo niliyoyapata kutoka kwa mwenyeji wangu huyo nilijua moja kwa moja wanakijiji wa kata ya jipendea hawana elimu ya kilimo.. na nikagundu kumbe ndio maana unakuta watu wanakopa fedha kutoka mashirika ya kukopesha mf:sacos mwisho wanashindwa kurejesha mkopo waliyokopa yote hayo ni kutokana na kukosa elimu ya kilimo.
Sasa kama mkulima anakopa kisha anashindwa kulipa mkopo huo je kunauwezakano wa kuwepo kwa maendeleo? jibu ni hapana. ila mimi napendekeza elimu lazima itolewe kwa wakulima, kumbuka kuwa mkulima ndio kiungo kikubwa tanzania na hata duniani. lakini leo hii mkulima anaechipukia kwa kilimo kisha mkamnyima elimu ya kilimo manategemea nini.?kazi kweni serikali..
katika sehemu nyinge naona ni bora hayo mashirika ya kukopesha kwanini yasitoe ushauri kwa wakulima wanaokopesha.. ikiwemo kushirikiana na ma bwana shamba kuwapa elimu na pia ushauri na kuwapa mfumo mzima wa kilimo cha kisasa..? lakini kinachoniuma mimi kama mwangajamii nipale mkulima mpaka leo anatumia jembe la mkono.. na sio. kuwa anapenda ni kwa sababu ya vifaa vya kisasa kuwa na gharama kubwa. na ukilinganisha na kipato cha mtu anaishie vijijini ni kidogo.. kiukweli labda mtu ana mlo mmoja kwa siku alafu umwambie maswala ya power tiler hawezi kukuelewa... hata akikopeshwa bado riba yake nikubwa na uwezi kumpa power tiler kama elimu hana ya kilimo.. cha muhimu ni serikali ya tanzania kuweka mkakati wa kupeleka ma bwana shamba wa kutosha na hao ma bwana shamba wawajibike na sio kula bata tu. leo hii mnatuambia oohh kilimo kwanza nahisi kama ni jocking kwa wananchi wa vijijini. na ukitazama Tanzania imebarikiwa maeneo makubwa. na inauwezo wa kusambaza chakula afrika nzima lakini uongozi hauko makini na rasilimali ya tanzania. ila wanafaidika watu wa nje. huku watanzania tukipiga mihayo ya njaa wengine wakila na kusaza.. Eti tanzania nchi yangu ingekuwa nchi yako usingekufa na njaa...
narudia tena KILIMO KWANZA 0% ila serika naomba ikaze buti kimaendeleo hususani ya kilimo...
6 Comments